IQNA – Qur’ani Tukufu inakataza waziwazi aina yoyote ya ushirikiano katika maovu au uonevu. Katika Surah Al-Ma’idah aya ya 2, Allah anasema: “Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”
IQNA – Mashambulio dhidi ya misikiti nchini Uingereza yameripotiwa kuongezeka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni, huku ripoti mpya ikihusisha ongezeko hilo na harakati za utaifa zinazotumia alama za Kikristo na za Uingereza katika vitendo vya vitisho.
IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimelaani mlipuko wa bomu uliotokea katika msikiti mjini Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, wakati wa Sala ya Ijumaa, na kujeruhi watu kadhaa.
IQNA – Katika mandhari ya vijijini vya Malawi, taswira za watoto wakishiriki kwa ari katika miduara ya kisomo cha Qur'ani Tukufu zimeanza kuvutia mitandaoni, zikidhihirisha mchango hai wa jamii ya Waislamu wachache nchini humo.
IQNA – Mtaalamu wa afya ya akili nchini Iran ameonya kwamba matumizi kupita kiasi ya mitandao ya kijamii yanawafanya vijana kujitenga, huku yakibadilisha maadili yao. Ameitaka jamii ya wazazi Waislamu kuamiliana na watoto kwa huruma, subira na mfano wa vitendo, si kwa kuwabana na kuwadhibiti.
IQNA-Operesheni ya pamoja ya kukabiliana na ugaidi kati ya Jamhuri ya Ireland na Ireland Kaskazini imefanikiwa kuzuia shambulio lililopangwa dhidi ya msikiti na vituo vya wahamiaji, na kupelekea kunaswa vilipuzi na kufikishwa mahakamani kwa wanaume wawili ambao sasa wanakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na tukio hilo.
IQNA-Katika ripoti mpya iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya Uswidi, imebainika kuwa idadi kubwa ya wanafunzi Waislamu wamekuwa wakihama shule kutokana na kukumbwa na ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu.
IQNA – Takriban watu 54 wamejeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea katika msikiti ulioko ndani ya eneo la shule jijini Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, siku ya Ijumaa, kwa mujibu wa taarifa za polisi wa eneo hilo.
IQNA-Ayatullah Alireza Aarafi, Mkurugenzi wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu (Hauzah) nchini Iran ametoa ujumbe mzito wa kulaani mauaji ya kikatili dhidi ya watu wanyonge wa Sudan, akiwataka Waislamu na taasisi za kimataifa kuchukua msimamo wa wazi na wa dhati kuwasaidia Wasudan wanaodhulumiwa
IQNA – Nyumba ya Makumbusho ya Sanaa za Kiislamu mjini Jeddah, maarufu kwa jina la Dar al-Funun al-Islamiyyah, imeandaa maonesho ya hati adimu za Qur’ani Tukufu pamoja na kazi za sanaa zinazodhihirisha uhusiano wa kihistoria kati ya imani ya Kiislamu, uzuri wa sanaa, na ustadi wa mikono.
IQNA – Mkutano wa 4 wa Kimataifa kuhusu Usanifu wa Misikiti wa mwaka 2025 uliofanyika mjini Istanbul, Uturuki, umesisitiza haja ya kufikiria upya nafasi ya misikiti katika jamii za kisasa.
IQNA-Katika kasri maarufu la Topkapi jijini Istanbul, utamaduni wa kale wa Kiislamu wa usomaji wa Qur'ani Tukufu umeendelea bila kukoma kwa karne nyingi. Usomaji huu wa kila siku, ulioanzishwa na Masultani wa Uthmaniyya, unaendelea hadi leo kama sehemu ya urithi wa kiroho na kitamaduni wa Waislamu wa eneo hilo.
IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimezindua awamu ya kwanza ya mashindano ya kila mwaka ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, maarufu kama Mashindano ya Sheikh Al-Azhar. Zaidi ya washiriki 150,000 wa kiume na wa kike kutoka mikoa mbalimbali ya Misri wanashiriki katika awamu hii ya mwanzo.
IQNA – Shorouk Marar ni mwanamke kutoka mji wa Beit Daqo, kaskazini-magharibi mwa al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, ambaye ana kisa cha azma thabiti na imani ya kina.
IQNA – Mwanazuoni mmoja amesema kuwa Bibi Fatima al-Zahra (AS) ndiye dhihirisho halisi la maana ya “Kawthar” kama ilivyoelezwa katika Qur’ani Tukufu, akimtaja kuwa ni chemchemi ya baraka za kiroho na maarifa ya kijamii, ambaye athari yake inaendelea kuunda fikra za Kiislamu hadi leo.