IQNA

Utamaduni wa Kiislamu

Msahafu ulioandikwa na wanakaligrafia wa kike wazinduliwa Iran

19:01 - January 12, 2024
Habari ID: 3478187
IQNA - Msahafu ambao umeandikwa na wanakaligrafia kadhaa wa kike wa Iran umezinduliwa katika mji wa Qom, Iran.

Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika siku ya Alhamisi katikati mwa jiji la Iran huku umati wa maafisa na wanazuoni wa kidini wakihudhuria.

Msahafu huo uimeandikwa na wanakaligrafia 26 wa kike huku mchakato huo ukichukua mwaka mmoja.

Mpango huo uliandaliwa na Darolketabeh ambayo ina uhusiano na Kituo cha Iran cha Uchapishaji na Usambazaji wa Qur'ani Tukufu.

Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom, Ayatullah Seyyed Hashem Hoseini Bushehri, alikuwa mmoja wa wazungumzaji waliobainisha kuwa kuandika Qur'ani na kusoma aya kunapaswa kufuatwa kwa kutekeleza miongozo yake.

"Kusoma na kutazama aya huleta thawabu kwa hakika lakini, thawabu kuu huja tunapoelewa dhana na kutekeleza kile inachosema," aliongeza mwanazuoni huyo.

Mwishoni mwa sherehe, wanakaligrafia walikabidhiwa zawadi kwa mchango wao katika mradi huo.

 

 

4193389

Kishikizo: kaligrafia
captcha