IQNA

Jinai za Israel

Mkuu wa Ansarullah: Viongozi wa Kiislamu wakabiliane na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina

21:30 - November 14, 2023
Habari ID: 3477890
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa harakati ya Mapambano ya Kiisalmu (muqawama) ya Ansarullah ya Yemen amezitaka nchi za Kiarabu na Ulimwengu wa Kiislamu kuwa na misimamo ya wazi katika kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Sayyid Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi alisema hayo katika hotuba ya televisheni iliyotangazwa moja kwa moja siku ya Jumanne kuadhimisha kumbukumbu ya "Mashahidi" katika mji mkuu wa Yemen wa Sana'a.

Israel imekuwa ikishambulia kwa mabomu Gaza tangu tarehe 7 Oktoba, baada ya harakati ya muqawama wa Palestina Hamas kuanzisha operesheni kubwa ya Kimbunga ya Al-Aqsa dhidi ya utawala ghasibu wa Israel ikiwa ni jibu la jinai za miongo kadhaa za  utawala huo katili dhidi ya Wapalestina.

Tangu Israel ianzishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, idadi ya vifo vya Wapalestina imefikia 11,400, wakiwemo watoto 4,609 na wanawake 3,100. Idadi ya majeruhi ilifikia 28,200, huku 70% wakiwa watoto na wanawake.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, wananchi 3,250 bado hawajapatikana au chini ya vifusi, wakiwemo watoto 1,700.

 Al-Houthi amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Israel unafanya mauaji ya kimbari huko Gaza na ulimwengu wa Kiislamu umeonyesha msimamo "dhaifu na wenye mipaka" kuhusu ukatili wa utawala huo ghasibu.

Kiongozi wa Ansarullah ameongeza kuwa: "Gaza inakabiliwa na mauaji ya kimbari na mauaji ya kinyama ya watu wake hata kwenye misikiti, shule, hospitali na katika makao ya mashirika ya kimataifa waliokimbilia hifadhi."

"Katika kukabiliana na janga kubwa ambalo watu wa Palestina wamekuwa wakikabiliwa nalo kwa zaidi ya miaka 70, zaidi ya Waislamu bilioni wemonyesha msimamo duni na dhaifu. Aliendeleza malalmiko yake kwa kusema. "Tawala za Kiarabu hazina nia ya kuchukua hatua kwa uzito kuhusiana  Gaza."

Al Houthi alisisitiza kuwa Ukanda wa Gaza unakabiliwa na mzingiro wa pamoja wa Israel na Waarabu, na nchi jirani hazijaribu kwa dhati kupeleka chakula, dawa, na misaada ya kibinadamu ambayo eneo hilo la kizuizi linahitaji.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni siku ya Jumanne, mkuu huyo wa Ansarullah pia alielezea kusikitishwa kwake na taarifa ya mwisho iliyotolewa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kiarabu  na Kiislamu mjini Riyadh mwishoni mwa juma.

Amesema: "Ingawa Mkutano wa kilele wa Nchi za Kiarabu na Kiislamu ulikuwa mkutano wa dharura wa nchi 57, haukuja na msimamo au hatua yaki vitendo, na hii ni aibu na ya kusikitisha."

“Mkutano wa kilele uliodai kuwawakilisha Waislamu wote ulitoa tu kauli zisizo na msimamo wa kiutendaji. Je, huu ndio uwezo huu wa Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu?” aliohoji na kuongeza kuwa, "Nchi hamsini na saba za Kiarabu na Kiislamu, pamoja na uwezo wao wote, zilitoka na taarifa ambayo ingeweza kutolewa na shule ya msingi na mtu mmoja."

Mkuu wa Ansarullah pia alisisitiza kwamba matokeo ya mkutano huo ni kauli "ya kawaida" ambayo "ilidhihakiwa na Waisraeli."

Al-Houthi alisisitiza kuwa msimamo wa watu wa Yemen katika suala la Gaza ni "imara," na akasema Sana'a itaendelea kutoa msaada na usaidizi kwa watu wa Palestina na wanamapambano wao hadi pale Palestina itakapokombolewa kutoka kwa uvamizi wa Israel.

4181858

Habari zinazohusiana
captcha