IQNA

Ukweli katika Qur'ani Tukufu /12

Qur’ani Tukufu inaashiria mabwawa ya maji matamu chini ya bahari

11:58 - March 06, 2023
Habari ID: 3476664
TEHRAN (IQNA) – Watafiti wa Australia wamethibitisha kwamba maji matamu yanaweza kupenya matabaka yaliyo katika kina cha na kubaki humo kwa zaidi ya miaka 20,000. Qur’ani Tukufu katika mojawapo ya aya zake imetaja jambo hili la kustaajabisha.

Wataalamu wamegundua kuwa kuna kiasi kikubwa cha hifadhi za matamu chini ya bahari zenye maji ya chumvi, na kukadiria kuwa kuna kilomita za ujazo nusu milioni za maji haya matamu ambayo yanatoka kila wakati.

Hii ni zaidi ya kiasi cha maji matamu ambayo wanadamu wametumia katika karne iliyopita.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Flinders huko Australia wanasema kiasi hiki cha maji kinaweza kukidhi mahitaji ya wanadamu kwa mamia ya miaka.

Swali ni jinsi maji haya matamu yanaweza kupenya maeneo ya maelfu ya mita chini ya uso wa bahari na kubaki huko kwa zaidi ya miaka 20,000? Qur’ani Tukufu inasema katika Aya ya 22 ya Surah Al-Hijr: "  Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka."

Aya hii inasema Mungu anateremsha maji kutoka mbinguni ambayo ni safi na matamu na yamehifadhiwa kwa njia ngumu ambayo wanadamu hawana uwezo wa kuifanya.

Nani amemjulisha Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kuhusu hifadhi ya maji matamu chini ya bahari? Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Aya ya 89 ya Surat An-Nahl: “…Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu,na rehema, na bishara kwa Waislamu.

captcha