IQNA

Ukweli katika Qur'ani Tukufu / 10

Je, At-Tariq ni nini?

12:48 - December 28, 2022
Habari ID: 3476318
TEHRAN (IQNA) - Kuna masuala mengi yanayohusiana na sayansi yaliyotajwa ndani ya Qur'an Tukufu ambayo yanachukuliwa kuwa muujiza wa Kitabu Kitukufu kwa sababu yalikuwa hayajulikani kwa wanadamu kwa muda mrefu na wanasayansi waliyagundua karne nyingi baadaye.

Tovuti ya I’ijaz al-Qur'ani (muujiza wa Qur'ani) katika makala imejadili vipengele vya muujiza vya aya tatu za kwanza za Sura At-Tariq ambayo ni sura ya 86 katika Qur'ani Tukufu.

“Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!. Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?  Ni Nyota yenye mwanga mkali.” (Aya ya 1-3)

At-Tariq ni kitu kilicho katika anga za mbali na kina sifa mbili: Ni nyota na inayopenya. Zaidi ya hayo, At-Tariq ina mipigo na hivyo ndivyo baadhi ya nyota za nyutroni hufanya. Baadhi ya nyota za nyutroni hutoa miale ya mionzi ya sumakuumeme inayozifanya zionekane kama nyota zenye mwanga mkali.

Nyota za nyutroni ni kati ya vitu vyenye unene zaidi katika anga za mbali. Ni nene kiasi kwamba ikiwa mmoja yao angeanguka ardhini, basi itajipenyeza katika kina cha ardhi.

Nyota za nyutroni huzunguka haraka sana, na mamia ya mizunguko kila sekunde. Ndio maana huunda uwanja wenye nguvu wa sumakuumeme na kutoa miale ya mionzi ya sumakuumeme. Hii inaunda sauti kama nyundo inayopiga kitu.

Wanasayansi wamerekodi sauti hizi, si moja kwa moja kwa sababu sauti haisafiri bila utupu, lakini kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia mawimbi ya redio yanayotolewa kutoka kwa nyota za neutroni.

Ni upendeleo wa Mwenyezi Mungu kwetu kwamba sauti haisafiri bila utupu kwa sababu la sivyo, sauti za nyota zingetufikia na tungekuwa viziwi.

captcha