IQNA

Jinai za Israel

Msikiti wa Al-Khalil washambuliwa na walowezi wa Israel

20:24 - February 20, 2023
Habari ID: 3476591
TEHRAN (IQNA) – Kundi la walowezi wa Kizayuni wameshambulia msikiti katika Mji Mkongwe wa Al-Khalil (Hebron), wakirusha mawe kwenye sehemu hiyo ya ibada ya Waislamu.

Walivunja madirisha yake na kuharibu uwanja wake siku ya Jumapili, vyanzo vya ndani vilisema.

Msikiti wa Sunia, ulioko katika eneo la Al-Sahla karibu na soko la mboga mboga, ulilengwa kama sehemu ya "jaribio la walowezi la kuwatisha waumini na kueneza hali ya hofu na woga miongoni mwao," Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu wa Al Khalil, Nidal Al- Jabari, alisema.

Ametoa wito wa kushadidishwa uwepo wa Wapalestina katika eneo hilo, na Wizara ya Wakfu ya Palestina iteue walinzi katika misikiti iliyo karibu na maeneo yenye mizozo licha ya hatari ya kushambuliwa na wanajeshi na walowezi haramu wa Israel.

Siku ya Jumapili asubuhi, walowezi pia waliwazunguka wachungaji wawili walipokuwa wakichunga kondoo wao katika eneo la Al-Maarajat, magharibi mwa Ariha (Jericho), na kuwatishia kwa silaha.

Hassan Malihat, msimamizi mkuu wa Shirika la Al-Baydar la Kutetea Haki za Wabedui, alisema kuwa walowezi wapatao 20 waliwazunguka wachungaji hao wawili, Ismat Atta Ka'abneh na Muhammad Suleiman Ka'abneh, walipokuwa wakichunga kondoo zao kwenye maeneo ya ufugaji huko. eneo la Arab Al-Mleihat kwenye barabara ya Al-Maarajat, na kuwalazimisha kuondoka eneo hilo.

3482543

captcha