IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje / 24

Qur'ani Tukufu inatazama msimamo wa wastani kuwa msingi mabadiliko

17:25 - October 22, 2022
Habari ID: 3475970
TEHRAN (IQNA) – Qur’ani Tukufu inasisitiza sana kuhusu kuepuka ubadhirifu kama njia ya kuboresha jamii, kuunda usawa na kuelekea kwenye wokovu katika jamii.

Msimamo wa wastani una nafasi maalum katika mtindo wa maisha wa Kiislamu. Ili kuelewa dhana hii ya kiutendaji maishani, itakuwa muhimu kuzingatia neno 'Israf'. Israf maana yake ni ubadhirifu na kutokuwa na wastani na kuzidihsa. Israf imetajwa mara 23 ndani ya Qur'ani, ikiwa ni pamoja na aya ya 31 ya Surah Al-A’raf:

“Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu."

Sababu ya kwa nini Mwenyezi Mungu hawapendi wafujaji ni kwa sababu Israf inaongoza kwenye ufisadi na kuharibika kwa kudhoofisha mizani katika kila kitu. Inaharibu mali na milki za mtu na kusababisha uhaba.

Aina za Israf

- Israf ya Kijamii

Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka, Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi. (Sura Ash-Shu’ara, aya ya 151-152)

Ufisadi wowote wa kijamii ukiwemo umwagaji damu, dhulma, kiburi na Istikbar , ni aina ya Israf inayovuruga mizani na jamii na kueneza migogoro, migogoro na changamoto.

2- Israfu ya kiakili

“…Kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha kupotea anaye pindukia mipaka katika maasi anaye jitia shaka. (Surah Ghafir, aya ya 34)

Shaka ni jambo la kawaida lakini kuwa na mashaka yasiyo na msingi kila wakati kunadhuru na kuzingatiwa kuwa ni aina ya Israf.

3- Tabia Israfu

“Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.’’ (Surah Az-Zumar, aya ya 53)

Aya hii inaitaja Israf dhidi ya nafsi yako, ambayo wafasiri wa Qur'ani Tukufu wanaitaja kuwa ni dhulma kwa nafsi yako.

4- Israf dhidi ya Wengine

Kutumia vibaya mali na milki za wengine, haswa zile za mayatima, inachukuliwa kuwa ni aina ya Israf na Qur'ani Tukufu inakataza kwa nguvu zote:

“Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri naajizuilie, na aliye fakiri basi naale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu." (Surah An-Nisa, aya ya 6)

5- Israfu katika Adhabu

 Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.” (Surah Al-Isra, aya ya 33)

Kutofanya kupita kiasi katika kuwaadhibu waliofanya makosa, wakiwemo wauaji, ni miongoni mwa mambo ambayo Uislamu unayatilia mkazo na kuyapuuza haya yamezingatiwa kuwa ni Israf.

6- Israfu katika Ulaji

 " Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu. " (Surah Al-A’raf, aya ya 31)

7-Israf katika Infaq (Sadaka)

" Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo. " (Surah Al-Furqan, aya ya 67)

Infaq katika njia ya dhambi, Infaq kwa unafiki na kujionyesha, na Infaq kupindukia ni miongoni mwa hatua zinazochukuliwa kuwa ni Israf katika Infaq.

captcha