IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje/27

Infaq; Kutoa sehemu ya kile unachopenda sana

10:47 - September 01, 2022
Habari ID: 3475714
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa aya ya Qur’ani Tuku, mtu anatakiwa kutoa sadaka au kupeana sehemu ya kile anachokipenda ili kufikia cheo cha watu wema.

Infaq maana yake ni kutoa sadaka au kutoa sehemu ya mali ya mtu kwa wale wanaohitaji. "Birr" ni neno la Qur'ani Tukufu linalorejelea haki, uchamungu, uadilifu na kila tendo la utiifu kwa Mwenyezi Mungu. Pia ni cheo kikubwa ambacho kimeahidiwa kwa wale wanaofanya mambo mema. Kulingana na baadhi ya riwaya, msimamo huo nyakati fulani hufafanuliwa kuwa ule wa wanadamu wanaostahili zaidi mbele za Mungu; Ahl al-Bayt (SA) yaani watu wa nyumba ya Mtume Muhammad SAW wako katika kundi hili.

Swali ni hili, ni nani anastahili kufurahia nafasi hii?

 “Kabisa hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua." (Qur'ani Tukufu, Sura Al Imran, aya ya 92)

Kwa mujibu wa aya hii, mojawapo ya masharti ya kupata nafasi ya watu wema ni kutoa na kutoa sehemu ya mali anayoipenda mtu.

Allamah Tabatabai, mfasiri maarufu wa  Qur'ani Tukufu aliyeandika Tafsi al Mizan, anamini kwamba mwanadamu anapenda kujilimbikizia mali kana kwamba hii ni sehemu ya maisha yake; upendo huu ni kwa kiasi kwamba ikiwa atapoteza sehemu ya mali aanahisi kuwa sehemu ya maisha yake imeharibiwa. Hii inaashiria umuhimu wa infaq kutoka kwa kile mtu anachokipenda kweli na akifanya hivyo hupelekea kufika kwenye nafasi ya “Birr”.

Wakati huo huo, mfasiri wa zama hizi wa Qur'ani Sheikh Mohsen Qara’ati ambaye ameandika Tafsir Nur anarejelea nukta 12 kuhusu aya hii:

  1. Njia pekee ya kufikia nafasi ya watu wema ni infaq kwa nia njema kutoka katika mali anayoipenda mtu
  2. Lengo la infaq katika Uislamu sio tu kuondoa umaskini bali pia ukuaji na ustawi wa nafsi ya mwenye kutoa
  3. Kusalimisha moyo wa mtu kwa ulimwengu kutawazuia watu binafsi kufikia nafasi ya 'Birr'
  4. Ukombozi wa watu binafsi unatokana na ukarimu wao na mtazamo wa kijamii
  5. Wanadamu hupenda maisha yao zaidi ya kitu kingine chochote hivyo mashahidi wafia dini wanaojitolea maisha yao katika njia ya Mwenyezi Mungu hufikia cheo cha juu kabisa cha Birr.
  6. Toa kile unachopenda, si kile ambacho maskini hupenda kwa sababu maskini anaweza kuridhika na vitu vya chini kwa sababu ya kuishi katika umaskini kwa miaka mingi.
  7. Ubora ni muhimu zaidi kuliko wingi katika infaq
  8. Uislamu unazingatia zaidi wanadamu kuliko vitu vya kidunia.
  9. Mtu anatakiwa kujiepusha na misimamo mikali wakati wa infaq kwani Qur'ani Tukufu insema “sehemu” ya kile anachokipenda kitolewe.
  10. Moja ya sifa za wanadamu ni tabia za kupenda lakini lililo muhimu ni ukubwa wa upendo huu, na hili linaweza kudhibitiwa na infaq.
  11. Kilicho muhimu hapa ni infaq haijalishi thamani yake ni kiasi gani.
  12. Mwenyezi Mungu anaangalia infaq yetu, kwa hivyo hatupaswi kupuuza kitendo hiki.
Habari zinazohusiana
captcha