IQNA

Harakati ya Qur'ani

Makumi ya maelfu katika mjumuiko mkubwa zaidi wa Qur’ani Iran

13:35 - March 27, 2024
Habari ID: 3478589
IQNA - Katika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Hassan Mujtaba (AS), mkusanyiko mkubwa zaidi wa wanaharakati Qur'ani Tukufu nchini Iran umefanyika katika Uwanja wa Azadi mjini Tehran wenye uwezo wa kubeba watu laki moja.

Hafla hiyo iliyofanyika siku ya Jumanne, ilipambwa na uwepo wa maelfu ya wapenda Qur'ani, pamoja na waandaji na wataalamu kutoka kipindi cha TV cha "Mahfel".

Mjumuiko huo ulianza shughuli zake kwa qiraa ya Qur’ani Tukufu ya  Hamed Shakernejad, qari wa Iran anayetambulika kimataifa, aliyesoma ya za Surah al-Insan. Baada ya hapo Ahmed Abolghasemi, qari mwingine alisoma aya za mwisho za Surah Baqarah. Wataalamu wa kipindi cha Mahfel TV kisha walijiunga naye kwa usomaji wa kikundi.

Katika kuongeza hamasa ya kipekee kwenye mkusanyiko huo, kulikuwa na qasida iliyosomwa na kundi la Najm al-Thaqib. Wakati tukio likiendelea, qari wa Iran Mahdi Gholamnejad aliwasilisha kisomo maalum akiwa pamoja na watoto wake.

Wakati wa kuhuzunisha katika mkusanyiko huo ulikuwa ni heshima iliyotolewa kwa watoto waliouawa kishahidi katika hujuma ya Israel inayoendelea huko wa Gaza. Hadhirina waliguswa sana masaibu wanaopata Wapalestina na waliwasomea Sura Fatiha mashahidi wa Gaza.

Hafla hiyo ya Qur'ani ilihutubiwa na kiongozi wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina Ziyad al-Nakhalah ambaye aliwapongeza wananchi wa Iran kwa uungaji mkono wao usioyumba kwa harakati za ukombozi wa Palestina. Aidha amesema nyoyo za Wapalestina daima ziko pamoja na Wairani kwani Qur'ani tukufu ndiyo inayowaunganisha watu wa mataifa haya mawili. Amesema Wapalestina wataendeleza mapambano yao hadi upatikane ushindi.

Tukio hilo lililenga kufasiri aya 30 katika Quran Tukufu. Mpango huu, unaojulikana kama "Kuishi na Aya," uliishia katika usomaji wa pamoja wa Qur’ani Tukufu uliojumuisha wote waliokuwa katika uwanja huo mkubwa zaidi wa soka nchini Iran.

Kampeni hiyo, iliyoratibiwa na muungano wa taasisi na wanaharakati wa Qur'ani, ilichagua aya 30 muhimu kutoka kwa Qur'ani Tukufu ambazo ni muhimu katika kuimarisha misingi ya kidini ya waliohudhuria.

Mjumuiko huo ulimalizika kabla ya Sala ya Magharibi ambao kulisambazwa milo 150,000 ya futari miongoni mwa hadhirina.

4207260

4207260

captcha