IQNA

Ukanda wa Gaza

Mjumuiko mkubwa wa futari Rafah pamoja na kuwepo hujuma ya Israel

16:02 - March 26, 2024
Habari ID: 3478586
IQNA – Mjumuiko mkubwa wa futari umefanyika katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, licha ya kuendelea mashambulizi ya utawala haramu Israel dhidi ya mji huo.

Wapalestina walijumuika kwa ajili ya futari katika mtaa mmoja wa Rafah ambapo mamia ya watu walishiriki..

Mpango huo wa iftar umefadhiliwa na baadhi ya Wapalestina wenyeji  wa Rafah kuwasaidia mamia ya wenzao ambao ni miongoni mwa milioni 1.4 ambao wamekimbilia katika mji huo ulioko kusini mwa Gaza.

"Tuliamua kuandaa futari ya pamoja, ya wali na nyama, pamoja na kuwepo vita," Musallam Ahmed, mmoja wa waandalizi wa futari, amesema.

"Lengo letu ni kuleta furaha kwa mioyo ya wale wanaofunga katika mazingira haya magumu ya kuzingirwa na vita, na kuwapa chakula kizuri na chenye lishe."

Hayo yanajiri kukiwa na maonyo ya kieneo na kimataifa kuhusu athari za uvamizi wowote wa nchi kavu ya Israel huko Rafah.

Utawala wa Israel uliidai kuwa ni salama kwa Wapalestina waliokimbia makazi yao kwenda Rafah, lakini kisha ukaanzisha mashambulizi ya angani dhidi ya mji huo ambayo yameua na kujeruhi mamia ya watu wakiwemo watoto na wanawake.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel Benjamin Netanyahu alitangaza tarehe 15 Machi kwamba ameidhinisha mipango ya kutekeleza operesheni ya kijeshi mjini Rafah.

3487717

Habari zinazohusiana
captcha