IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Misri ya kuwakutanisha waliobobea zaidi

16:51 - February 13, 2024
Habari ID: 3478346
IQNA - Mashindano ya kimataifa ya mabingwa katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu na utamaduni wa Kiislamu yamepangwa kufanyika nchini Misri msimu huu wa kiangazi.

Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Mohammed Mukhtar Gomaa alisema Jimbo la Sinai Kusini la nchi hiyo litaandaa mashindano hayo.

Alisema hayo katika mkutano na gavana wa Sinai Kusini siku ya Jumatatu, tovuti ya Cairo24 iliripoti.

Kwa mujibu wa Wizara ya Wakuf, tukio hilo la Qur'ani linalenga kuhimiza vipaji vya Qur'ani kutoka nchi mbalimbali na kutangaza utamaduni wa Kiislamu.

Pia inalenga kuwafahamisha washiriki kuhusu uzoefu wa Misri katika kutumikia Qur'ani Tukufu, ilisema.

Washiriki watashindana katika sehemu nne zifuatazo:

Kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa wanaume (chini ya miaka 35) ambao wameshinda nafasi ya kwanza au ya pili katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yenye itibari.

Kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa wanawake (chini ya miaka 35), ambao wameshinda nafasi ya kwanza au ya pili katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yenye itibari.

Kuhifadhi Qur'ani kwa vijana wakubwa (chini ya miaka 15) ambao wameshinda nafasi ya kwanza, ya pili au ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yenye itibari.

Utamaduni wa Kiislamu kwa wale walio na umri wa chini ya miaka 40 ambao waliwahi kushika nafasi kwanza au ya pili katika kategoria kama vile tafsiri ya Qur'ani, Seerah ya Mtukufu Mtume (SAW), na usomaji wa Ibtihal katika mashindano nchini Misri.

Mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani ya mabingwa wa Qur'ani yatafanyika tarehe 12 Julai 2024.

3487170

captcha