Kwa mujibu wa riwaya Sama’a ibn Mihran anasema idadi kadhaa ya watu walikuwa pamoja na Imam Sadiq (AS) wakati mada ya hekima na ujinga ilipokuja.
Imamu Sadiq (AS) amesema: Ijueni akili (hekiman) na jeshi lake na pia jueni ujinga na jeshi lake ili mpate kuongoka.
Sama’a anasema Imam Sadiq (AS) alifafanua kwanza akili au hekiman na ujinga na kisha akataja sifa 75 za jeshi la akili na 75 za jeshi la ujahilia.
Imamu Sadiq (AS) ameongeza kuwa Mitume wa Mwenyezi Mungu, watu wa Mwenyezi Mungu na kila muumini wa kweli wamejizatiti kwa jeshi la wenye hekiman..