IQNA

Jinai za Israel

Gaza yashambuliwa na Israel, takriban Wapalestina 198 wauawa

22:32 - October 07, 2023
Habari ID: 3477699
TEHRAN (IQNA) – Jeshi katili la Israel siku ya Jumamosi lilianzisha mashambulizi ya anga kwenye Ukanda wa Gaza, na kuua Wapalestina wasiopungua 198, wakiwemo wanawake na watoto, katika eneo hilo.

Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imeripoti kuwa watu 198 wameuawa na takriban 1,610 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Utawala wa kikoloni wa Israel unaendesha mashambulizi ya anga katika ardhi ya Palestina baada ya wapigania ukombozi wa Palestina mapema Ijumaa kuanzisha operesheni yao kubwa zaidi dhidi ya Israel katika kipindi cha miaka mingi katika mashambulizi ya kushtukiza ambayo yalihusisha wapiganaji waliovuka uzio na kuingia katika miji ya Paestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel ambapo wamevurumisha mamia ya maroketi kutoka Ukanda wa Gaza.

Takriban Waisraeli 250, wengi wakiwa ni askari wa jeshi katili la Israel na walowezi wa Kizayuni wameuawa na zaidi ya 1000 kujeruhiwa, vyombo vya habari vya Israel viliripoti, ikinukuu huduma ya ambulensi ya Israel.

Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, Salah Arouri alisema Kimbunga cha Al-Aqsa ilikuwa jibu "kwa uhalifu wa uvamizi." Amesema wapiganaji wameanzisha vita kwa ajili ya kiulinda Msikiti wa Al-Aqsa huko al-Quds (Jerusalem) ambao umekuwa ukihujumiwa mara kwa mara na Israel. Aidha amesema oparesheni hiyo inalena kuwakomboa maelfu ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa mateka na Israel.

Kamanda mwandamizi wa jeshi la Hamas Mohammad Deif alisema, "Hii ni siku ya vita kubwa zaidi kumaliza ukaliaji mabavu wa mwisho duniani."

Alisema wapigania ukombozi wa Palestina walishambulia maeneo mengi ya Israel, vikiwemo viwanja vya ndege na vituo vya kijeshi.

3485466

Habari zinazohusiana
captcha