IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Kikao cha Kimataifa Qatar chataka hatua za kukabilina na chuki dhidi ya Uislamu

18:50 - October 02, 2023
Habari ID: 3477683
TEHRAN (IQNA) -Mkutano wa kimataifa kuhusu chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) umefanyika nchini Qatar huku mmoja wa waandalizi wake akitoa wito kwa juhudi za pamoja za kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na athari zake "haribifu".

Mkutano huo uliopewa anuani ya "Historia ya Ulimwengu na Mienendo ya Chuki dhidi ya Uislamu," umefanyika katika Chuo Kikuu cha Georgetown tawi la Qatar

Katika hotuba ya kuhitimisha Jumapili., Mkuu wa Chuo Kikuu cha Georgetown Qatar Safwan M. Masri aliashiria haja ya juhudi za pamoja.

Alisema kuwa tukio hilo limetoa "mchango katika juhudi za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu, kupinga athari zake haribifu, na kuchukua hatua athirifu zinazojumuisha wanaharakati, waelimishaji na wasanii ili kukabiliana na tatizo hilo.

Washiriki katika hafla hiyo ya siku mbili walijishughulisha na mazungumzo, waliuliza maswali, na kuchunguza mizizi ya kiitikadi ya mielekeo mingi ya chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu.

Kongamano hilo lileta pamoja "wasomi wenye ushawishi mkubwa, watendaji, na waandishi wa habari, kati yao wanafunzi wa zamani wa Georgetown na wanafunzi wa Qatar wa Chuo Kikuu cha Georgetown ambao wamechangia ufahamu wao," taarifa kwa vyombo vya habari inasoma.

"Mkutano huo uliishia katika mjadala wa ngazi ya juu wa meza ya pande zote ambapo washiriki wamechunguza suluhu zinazowezekana ili kupambana na chuki dhidi ya Uislamu."

Washiriki walisema pamoja na Uislamu kuwa neno la kawaida katika muongo mmoja uliopita, ni wajibu kwa wasomi na watendaji kuchunguza historia ya chuki dhidi ya Uislamu ili kuelewa tatizo hilo kikamilifu.

3485403

Habari zinazohusiana
captcha