IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Mwanazuoni wa Lebanon: Serikali za Kiislamu zichukue hatua kuzuia kuvunjiwa heshima Qur'ani

18:34 - August 10, 2023
Habari ID: 3477412
BEIRUT (IQNA) - Mwanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon alisisitiza haja ya serikali za Kiislamu kuchukua hatua ili kuzuia kurudiwa kwa kunajisi Qur'ani nchini Uswidi na Denmark.

Sheikh Ibrahim al-Baridi, msomi wa Kisunni na katibu wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon, aliiambia IQNA katika mahojiano kwamba kunajisi matakatifu ya kidini kamwe hakuwezi kuhalalishwa kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Wala haiafikiani katika sheria yoyote, alisema, akisisitiza kuwa serikali ya Uswidi imekiuka sheria kwa kutoa idhini kwa baadhi ya watu kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini humo.

Sheikh al-Baridi alisisitiza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mlinzi wa Uislamu na utakatifu wake na wale wanaodhani wanaweza kuidhoofisha dini na Quran wamekosea.

Wale wanaoichoma Qur'ani wanatafuta kudhoofisha maadili ya Kiislamu lakini moto wa Fitna ( fitna hii) utazimwa, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (katika Aya ya 64 ya Surah Al-Ma'idah) " Kila mara wanapo washa moto wa vita, Mwenyezi Mungu anauzima.”

Mwanazuoni huyo wa Lebanon aliendelea kusema kuwa, iwapo vitendo vya kuivunjia heshima Uswidi na Denmark vitaendelea, serikali za nchi za Kiarabu na Kiislamu zinapaswa kuchukua misimamo dhidi ya serikali za nchi hizo

Sheikh Al-Baridi alibainisha zaidi kwamba nchi hizo za Ulaya zina maslahi katika nchi za Kiislamu (na ili kuzilinda) zinapaswa kuzuia matukio ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Katika wiki za hivi karibuni, kuchafuliwa kwa Qur'ani nchini Uswidi na Denmark kwa idhini ya serikali na ulinzi wa polisi kumezua hasira  katika ulimwengu wa Kiislamu.

4160610

Habari zinazohusiana
captcha