IQNA

Harakati za Qur'ani

Wanafunzi milioni moja wajiandikisha kwa kozi za Qur'ani Tukufu nchini Algeria

23:11 - May 05, 2023
Habari ID: 3476961
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Masuala ya Kidini wa Algeria amesema baadhi ya wanafunzi milioni moja wamejiandikisha kwa ajili ya kozi za Qur'ani nchini humo.

Katika hotuba yake pambizoni mwa kongamano la shule za kuhifadhi Qur'ani mjini Algiers, Youcef Belmehdi amesema kozi hizo zinafanyika katika shule 18,000 za Qur'ani kote katika nchi hiyo.

Akiashiria umuhimu unaohusishwa na elimu ya Qur'ani nchini Algeria, alisema mikoa 50 ya nchi hiyo ina bodi za kufundishia usomaji wa Qur'ani.

Alisema bodi hizo zina wajumbe kati ya 5 hadi 25, ambao baadhi yao wana ustadi wa mbinu 10 za usomaji wa Qur'ani Tukufu.

Belmehdi alibainisha zaidi kwamba wanafunzi 50,000 wa Qur'ani walishiriki katika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani nchini humo wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, baadhi ya washiriki akiwemo Abdul Latif Bu Azizi kutoka Tunisia na Sheikh Hassan Bursu kutoka Senegal walienziwa.

Algeria ni nchi iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo ambayo huwa na harakati mbali mbali za Qur'ani Tukufu.

 

4138507

captcha