Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni wakati maalum wa mwaka ambao Waislamu kote ulimwenguni wanapaswa kufunga kuanzia mwanzo wa mwezi. Kwa wale wanaoishi katika nchi za Kiislamu, ambapo watu wengi hufunga wakati wa mwezi wa Ramadhani, ni rahisi kuzingatia mila na desturi za mwezi huo. Lakini inaweza kuwa vigumu zaidi kwa Waislamu wanaoishi katika nchi zisizo za Kiislamu. Hapa tunanukulu tovuti ya Al Bawaba ambayo imechapisha orodha ya apu au aplikesheni ambazo zinaweza kutumiwa na Waislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
1 – Turathi ya Ramadhani (Ramadan Legacy)
Hii ni mojawapo ya programu au apu maarufu zaidi zinazohusiana na Ramadhani na hukuruhusu kushiriki maudhui yako na kuona maudhui ya wengine katika Mwezi wa Ramadhani. Pia hukuwezesha kupanga shughuli za kibinafsi kwa muda wa siku 30. Aidha apu hii maktaba iliyojaa vidokezo na miongozo ya Ramadhani.
2- Kupika Chakula cha Halal (My Halal Chicken)
Kwa wale wanaoishi nje ya nchi za Kiislamu, kupata chakula cha halali ni vigumu. Ikiwa huna uzoefu mkubwa katika kupikia, hali hii inakuwa mbaya zaidi. Hapa ndipo apii hii inakuwa na manufaa makubwa. Apu hii inaweza kuwa mwongozo wako wa kupika vyakula ambavyo kila mtu anapenda kula.
3- Zabiha
Ikiwa kupika sio jambo lako, hiyo haimaanishi kuwa huwezi kula kitu kilichotengenezwa na mpishi wa kitaaluma. Zabiha ni programu inayokusaidia kupata migahawa ya Halal kwa urahisi, ambayo inaweza kuwa jambo la lazima kwa Waislamu wote ambao hawana muda wa kupika.
4 - Msomaji wa Qur’ani (Qur’an Reader)
Programu hii ni muhimu kwa Waislamu ambao hawajui lugha ya Kiarabu au kusoma Kiarabu kwa sababu inawaruhusu kubofya mstari wowote wa Qur’ani Tukufu na apu itawasomea aya. Aidha wanaojua kusoma Kiarabu wanaweza kusoma Qur’ani moja kwa moja katika apu hii ambayo pia inarajuma za Qur’ani kwa lugha mbali mbali za dunia. Api hii ni muhimu kwa Waislamu ambao hawajui Kiarabu vizuri wakati wa Ramadhani na itawafaidi hata baada ya mwezi huu mtukufu.
5 - Lishe katika Ramadhani (Ramadhan Diet)
Kwa wale wanaotarajia kupunguza uzito wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, apu hii inaweza kuwasaidia. Apu hii huwapa watumiaji shajara ya chakula inayowaambia nini cha kula na kile wasichopaswa kula, pamoja na kuwapa watu vidokezo na maagizo. Hatimaye, inawakumbusha watumiaji wakati wa kula na wakati wa kufanya mazoezi ikiwa wamesahau kufanya hivyo.
4128382