IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Shindano la Kimataifa la Qur’ani Tukufu Algeria wazawadiwa

22:06 - February 19, 2023
Habari ID: 3476583
TEHRAN (IQNA) - Washindi wa Shindano la 18 la Kimataifa la Kuhifadhi Qur'ani Tukufu Algeria wametunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika Jumamosi.

Jumla ya wahifadhi  51 wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali walishiriki katika shindano hilo, ambalo liliandaliwa kuanzia tarehe 6 hadi 17 Februari.

Shima Anfal Tabani kutoka nchi mwenyeji alishinda tuzo ya juu katika toleo hili huku mshindi wa pili akiwa Hassan Shuaib Shafei kutoka Sweden naye Abdul Aziz Makhlouf Salem Malouqa kutoka Libya alishika nafasi ya tatu.

Hafidh wa Qur'ani Tukufu  Abolfazl Aqdasi aliwakilisha Jamhuri ya Kiislamu katika mashindano hayo ya kimataifa.

Maafisa kadhaa wa serikali na wanadiplomasia kutoka nchi za Kiislamu walihudhuria hafla ya kufunga iliyofanyika katika mji mkuu Algiers.

Katika hotuba yake, Waziri wa Masuala ya Kidini na Wakfu Algeria Youssef Belmahdi alisema kuwa, kuandaa shindano hilo la  kimataifa ya Qur'ani Tukufu kunaashiria dhamira ya mataifa ya Algeria na mataifa mengine ya Kiislamu ya kufungamana na Qur’ani Tukufu na Uislamu.

Pia alishukuru msaada kutoka kwa rais wa Algeria na wasomi kwa mashindano hayo.

Afisa huyo alisisitiza zaidi uungaji mkono wa nchi hiyo ya Kiarabu kwa haki duniani, hasa kwa ajili ya Palestina.

Shindano La kimataifa ya Qur'ani ambalo lilianzishwa mwaka wa 2004 nchini Algeria hufanyika kila mwaka kwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha vijana walio chini ya umri wa miaka 25.

4122886

captcha