IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje /42

Aya ndefu zaidi ya Qur'ani Tukufu inahusu nini?

15:04 - December 25, 2022
Habari ID: 3476303
TEHRAN (IQNA) – Aya ndefu zaidi katika Qur’ani Tukufu inahusu masuala ya kisheria na jinsi ya kutengeneza nyaraka za biashara. Aya hii inaashiria jinsi Uislamu ulivyo mpana na jinsi unavyozingatia maelezo na kuandika mapatano.

Aya ya 282 ya Surah Al-Baqarah ndio aya ndefu zaidi katika Quran:
“Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.”
Maudhui ya aya yako wazi na hayahitaji maelezo. Wakati ambapo katika Bara Arabu kulikuwa na watu wachache walioweza kusoma na kuandika, msisitizo mkubwa wa uandishi unaonyesha umakini wa Uislamu kwenye elimu na kudumisha haki. Pia inaonyesha ufahamu wa dini na umakini kwa maelezo.
Tunnaweza kujifunza kutokana na aya hii kwamba watu katika jamii ya Kiislamu lazima wasaidiane katika kuheshimu haki.
Ujumbe wa aya ya 282 ya Surah Al-Baqara ni pamoja na:
1.    Kipindi cha deni kiwe wazi.
2.    Ili kudumisha kuaminiana na ili kutosahau deni, inapaswa mapatano yaandikwe.
3.    Ili kuhakikisha kuwa hakutakuwa na upotoshaji katika hati, iandikwe mbele ya mtu wa tatu.
4.    Anayeandika hati anapaswa kuwa mtu mwadilifu na mwadilifu.
5.    Kila mtu ana jukumu katika uwanja ambao ni mjuzi. Mwenye kalamu (na ni mjuzi wa kuandika) awaandikie watu.
6.    Mwenye deni atamke anachoandika mwandishi sio aliyetoa mkopo.
7.    Wakati wa kuandika mkataba, mwenye deni lazima amkumbuke Mwenyezi Mungu na awe mwangalifu asisahau chochote kuhusu deni.
8.    Kuzingatia mahitaji ya watu wasijiweza ni muhimu kwa viongozi.
9.    Wanaume wana kipaumbele juu ya wanawake katika kutoa ushahidi.
10.  Mashahidi wawe waadilifu na waaminifu na wenye kuaminiwa na pande mbili.
11.  Kiasi cha pesa kinachohusika sio muhimu lakini cha muhimu ni kulinda haki za watu.
12.  Kuandika hati kwa usahihi na kwa uadilifu na haki kuna faida tatu:
      I.        Kunahakikisha haki.
    II.        Inawapa mashahidi ujasiri wa kushuhudia.
   III.        Huzuia mashaka na kutoaminiana katika jamii.
13.   Mwandishi na shahidi hawaruhusiwi kuandika hati kwa namna ambayo itadhuru upande  mmoja.
14.   Mwandishi na shahidi ni walinzi wa haki za watu, na ikiwa watashindwa kulinda haki, itakuwa ni uadui.

captcha