IQNA

Kanuni za Imani za Kiislamu; Ufufuo/2

Dalili za mwelekeo wa kimaumbile wa mwanadamu kuelekea Ufufuo

22:44 - November 21, 2022
Habari ID: 3476125
TEHRAN (IQNA) – Wanadamu wana jibu la ndani kwa swali kuhusu hatima yao na maisha ya baadae na jibu hili linaweza kuonekana kupitia baadhi ya dalili zilizo wazi.

Ingawa baadhi ya watu hawakubaliani na maisha ya baada ya kifo na ufufuo, wana hisia ya maisha ya milele katika dhati ya nafasi zao na wanaonyesha ishara za itikadi hii ya maisha ya baada kuaga dunia.

Hii ni mifano:

  1. Wengi wa wanaokanusha ufufuo wanaheshimu makaburi ya mababu zao
  2. Wanaipa mitaa, majengo, shule n.k majina ya walioaga dunia.
  3. Wote wanapenda jina lao lihusishwe na ukumbusho mzuri baada ya kifo chao
  4. Wanawapa watoto wao majina ya wema
  5. Wengine miongoni mwao huhifadhi miili ya waliofariki ili isioze.

Iwapo wanaokanusha ufufuo wanakichukulia kifo kuwa ndio mwisho wa wanadamu, mtu anawezaje kuhalalisha vitendo hivi? Kwa vile wao huona kifo kuwa mwisho, hivyo huona kuwaheshimu wafu kuwa hakuna maana. Lakini pamoja na hayo,  kwa nini wanajenga makaburi ya wafu na kuwatolea maua au kuipa mitaa majina yao? Yote haya yanaonyesha kwamba wanaokanusha ufufuo wana imani kuhusu ufufuo  katika kina cha nafsi zao (ingawa ni dhaifu).Pia wengi wanaokanusha ufufuo wanaamini kuhusu roho, ubinadamu, na tabia ya wanadamu ambayo haitaangamizwa baada ya kufa.

Ndani ya dhati za nafsi zao na katika hisia zao za kimaumbile, wanadamu wanahisi kuna maisha baada ya kifo. Wakati huohuo, wanahisi pia kwamba ulimwengu huu hauwezi kujibu mahitaji yao yote na kwa njia fulani hawajisikii kuwa nyumbani. Wanaweza kujifurahisha kwa muda na mali, wenzi wa ndoa, na watoto, lakini baada ya muda, wanahisi kwamba ustawi huo wote haukidhi mahitaji yao.

Wanazua maswali kuhusu lengo la uumbaji, na sababu ya kuwepo kwao duniani. Hisia hizi zote zinaonyesha kuwa ulimwengu huu ni mdogo sana kwa roho kubwa ya wanadamu. Hili hutayarisha msingi wa kuamini siku ambayo wanadamu wanaweza kukidhi matakwa yao yote kwa sababu jibu la mahitaji yoyote ya ndani linaweza kupatikana nje  ya dunia hii.

 

Makala haya yametolewa kutoka katika kitabu kilichoandikwa na mwalimu na mtafiti wa Qur'ani wa Iran Hujjatul Islam Mohsen Qara'ati.

Kishikizo: ufufuo kanuni za imani
captcha