IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje / 35

Mtazamo wa Qur'ani kuhusu majukumu ya gharama za maisha

15:57 - November 16, 2022
Habari ID: 3476099
TEHRAN (IQNA) – Qur’ani Tukufu inatilia maanani sana familia, kitengo kidogo zaidi cha kijamii, na imechota haki za usawa za wanaume na wanawake. Moja ya haki hizo ni kukidhi gharama za maisha na Uislamu umewapa wanaume jukumu hili.

Wanaume na wanawake wana haki ambazo zimefafanuliwa kulingana na uwezo na mahitaji yao. Qur'ani Tukufu  hata imeleta baadhi ya haki kwa wanawake baada ya kufiwa na waume zao.

 “Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumba. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu kwa waliyo jifanyia wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” (Sura al Baqarah, aya ya 240)

Aya hii ni mfano wa wazi wa namna Qur'ani Tukufu inavyotilia mkazo jukumu la mwanaume kukidhi mahitaji ya mke wake.

Katika mtindo wa maisha ya Kiislamu, mwanamume ana wajibu wa kukidhi gharama za maisha ya mke na watoto

 “Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa.” (Surah An-Nisa, aya ya 34)

Mfasiri na mwalimu wa Qur'ani Tukufu Sheikh Mohsen Qara’ati anatoa baadhi ya pointi kuhusu aya zilizotajwa kutoka kwenye  aya ya 240 ya Surah al-Baqarah.

1- Wanaume wawache wake zao mali.

2- Mustakabali wa wajane uwe salama.

3- Uamuzi wowote wa mjane kuolewa na mwanamume mwingine uwe na msingi wa akili

4- Kanuni zilizoletwa ndani ya Qur'ani zinatokana na hekima ya Mwenyezi Mungu.

captcha