IQNA

Umoja wa Kiislamu

Sheikhe Mkuu wa Al-Azhar aalikwa kuitembelea Iran

16:39 - November 13, 2022
Habari ID: 3476081
TEHRAN (IQNA) – Hujjatul Islam Hamid Shahriari wa Iran amemwalika Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar Misri Sheikh Ahmed al-Tayyib kutembelea Iran kwa ajili ya mazungumzo kuhusu umoja wa Waislamu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa la Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST) Hujjatul Islam Hamid Shahriari ametoa wito huo wakati wa mahojiano ya Ijumaa na kituo cha televisheni cha Almayadeen Arabic TV.

Pia alisema yuko tayari kuchukua hatua ya kwanza kwa kutembelea Misri. "Pia tuko tayari kusafiri hadi Cairo na ujumbe kutoka Jumuiya ya  Kimataifa la Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ili kuzungumza na Sheikhe wa Al-Azhar na kujifunza mazungumzo ya Waislamu na Waislamu."

"Kumwalika mkuu wa Al-Azhar kunaongeza suala muhimu kwenye milinganyo kwani tunaweza kupinga na kutetea njama za maadui zinazolenga kuzusha mifarakano miongoni mwa Waislamu," Hujjatul Islam Shahriari alisema.

Iran inaunga mkono mwaliko wowote wa kuunda na kuimarisha umoja katika ulimwengu wa Kiislamu, amesisitiza mwanazuoni huyo.

Nyuma mnamo Novemba 7, Hujjatul Islam Shahriari alimuandikia barua  Sheikh al-Tayyib, alikaribisha wito wa mwanazuoni huo wa Kimisri wa mazungumzo ya Shia-Sunni.

"Kuonyesha utayari wako wa kuandaa mazungumzo haya pamoja na kuwepo kwa wanazuoni wa Al-Azhar kunaonyesha utayari wako katika suala hili na kwamba unatafuta kufikia malengo haya kwa uaminifu na nia safi na kwa lengo la kumwendea Mungu," aliandika.

WPFIST daima imekuwa ikitoa sauti yake ya kuunga mkono "wito wa ustaarabu na upainia" kwa kuweka tofauti kando na kuzingatia "maslahi ya Ummah" juu ya masilahi ya kibinafsi, aliongeza mwanazuoni huyo wa Kishia.

Akizungumza hivi karibuni nchini Bahrain, Sheikh el-Tayyib alisema: “Mimi na wanazuoni wakubwa wa Al-Azhar na Baraza la Wazee wa Kiislamu tuko tayari kwa mikono miwili kuketi pamoja kwenye meza moja ya duara na ndugu zetu wa Kishia ili kuweka kando tofauti zetu na kuimarisha umoja wetu wa Kiislamu.”

Mazungumzo hayo, alisema, yatalenga kufukuza  chuki, uchochezi na kutengwa na kuweka kando migogoro ya zamani na ya sasa.

"Natoa wito kwa ndugu zangu, wanazuoni wa Kiislamu, kote ulimwenguni wa kila itikadi na madhehebu kufanya mazungumzo ya Kiislamu," Sheikh al-Tayyib alisisitiza.

Alikuwa akizungumza katika kongamano lilofanyika Bahrain na kuhudhuriwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ambaye alifanya safari yake ya kwanza kabisa katika eneo la Ghuba ya Uajemi wiki hii.

3481223

captcha