IQNA

Uungaji mkono Palestina

Mashabiki wa Zamalek ya Misri wapata umashuhuri mitandaoni kwa kuunga mkono Palestina

15:50 - August 21, 2022
Habari ID: 3475660
TEHRAN (IQNA) – Picha za kuunga mkono Palestina zilizoonyeshwa na mashabiki wa timu ya soka ya Zamalek ya Misri zimesambaa miongoni mwa watumiaji wa Kiarabu wa mitandao ya kijamii.

Wakati wa mechi ya hivi majuzi kati ya timu za Zamalek na Pharco, wafuasi wa Zamalek walipeperusha na kuinua bendera za Palestina.

Katika mechi hiyi ya Ijumaa, Zamalek ilishinda Pharco 1-0, kulingana na tovuti ya Ray Al-Youm.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekaribisha hatua hiyo, wakisisitiza kuwa sababu ya Palestina itasalia katika mioyo ya raia wa Kiarabu milele.

Karim Yahya, mwandishi wa habari, amewapongeza mashabiki wa klabu hiyo ya michezo na kusema idadi kubwa ya Wamisri wanawaunga mkono watu wa Palestina na wanapinga uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amesema picha hizo pia zinathibitisha kulaani kwa Wamisri kwa mashambulizi ya utawala wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Ukweli kwamba vijana wa Misri wanasimama na Palestina na mapambano yao ni jambo ambalo haishangazi, aliongeza.

Wengi wa wale wanaotoa maoni katika mitandao ya kijamii kwenye picha walisisitiza kwamba kutegemea kuhalalisha uhusiano na Israeli katika eneo hakutakuwa na matokeo mengine isipokuwa kushindwa.

Walisisitiza kuwa Israel itasalia kuwa adui wa ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu licha ya jitihada za baadhi ya watawala kuanzisha uhusiano na utawala huo bandia wa Israel.

4079239

captcha