Haya ni kwa mujibu wa Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia. Waislamu ambao hawajachanjwa wanaruhusiwa kuingia kwenye Masjid al-Haram na Al-Masjid an-Nabawi kwa ajili ya Sala na Hija ndogo ya Umrah kwa sharti kwamba hawajaambukizwa au hawajawasiliana na mgonjwa wa COVID-19, wizara hiyo ilisema
"Watu ambao hawajachanjwa wameruhusiwa kusali katika misikiti miwili mitakatifu na kupata vibali kupitia programu ya Eatmarna kufanya Umrah, mradi hawajaambukizwa au kuwasiliana na mgonjwa wa COVID-19," ilieleza.
Msimu mpya wa Umrah ulianza Jumamosi, kwa mnasaba wa tarehe Mosi Muharram ambayo ni mwanzo wa mwaka mpya wa Kiislamu wa Hijiri.
Mamlaka katika ufalme huo zimejipanga kwa msimu mpya unaotarajiwa kuvutia zaidi ya Waislamu milioni 10, kulingana na maafisa wa Saudia.
3479947