IQNA

Muqawama

Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen aipongeza Hezbollah ya Lebanon kwa kuwa mfano

19:04 - July 31, 2022
Habari ID: 3475562
TEHRAN (IQNA) - Mwanachama mwandamizi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen Mohammad Ali al-Houthi amempongeza Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayed Hassan Nasrallah kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 40 ya kuasisiwa kwa harakati hiyo ya mapambano (muqawama) ya Kiislamu ya Lebanon.

Katika hotuba siku ya Jumamosi, Ali al-Houthi aliipongeza Hezbollah na katibu mkuu wake kwa kuwa kigezo bora zaidi katika kipindi cha miaka 40.

Amesema watu wa Yemen, kwa uimara na uthabiti wao katika kipindi cha miaka 8 iliyopita, ulijumuisha mfano mzuri wa ushindi, na kuongeza kuwa ndivyo wapigania uhuru wa Palestina, Iraq, Syria na Hezbollah walivyofanya.

Kuhusu suala la baadhi ya madola ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel, mwanasiasa huyo mwandamizi wa Yemen alisema kwamba "madhalimu wenye kiburi wanajaribu kuudhalilisha Umma wa Kiislamu (taifa) kwa kupigia debe uanzishwaji uhusiano na utawala wa Israel ambao unakiuka matukufu ya Waislamu.

Harakati ya Ansarullah iliilaani vikali Saudi Arabia mwezi uliopita kwa kuwaruhusu Wazayuni na Mayahudi kuingia Makka na Madina mwaka huu na kuvunjia heshima ibada ya Hija, na kusisitiza kuwa, "uwezeshaji unaotolewa na utawala wa Saudia kwa Mayahudi umekuja katika wakati ambapo mamilioni ya mahujaji wamezuiwa kutekeleza ibada hiyo. Hajj.”

Katika taarifa yake, harakati hiyo imeongeza kuwa, "ziara ya mwandishi wa televisheni ya Kizayuni huko Makka na Mlima Arafat, na pia maeneo mengine matukufu, ni shambulio la wazi dhidi ya matukufu ya Kiislamu na uchochezi kwa hisia za Waislamu."

3479911

captcha