IQNA

Sala ya Ijumaa Tehran

Ghadir ni ishara ya ukamilifu wa dini ya Uislamu na ramani ya njia ya jamii

23:15 - July 15, 2022
Habari ID: 3475506
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Suala la Ghadir ni kadhia ya kipekee katika historia ya mwanaadamu, na Mwenyezi Mungu hajalipa tukio lolote lile umuhimu mkubwa kuliko tukio la Ghadir Khum.

Tarehe 18 Dhulhijah inayosadifiana na Julai 18, 2022, inatambuliwa kuwa ni sikukuu ya Ghadir Khum ambayo ni mojawapo kati ya sikukuu kuu za Kiislamu.

Ghadir Khum ni jina la eneo kati ya Makka na Madina ambako Mtume Muhammad (SAW) wakati wa Hija yake ya Mwisho, alimtangaza Imam Ali bin Abi Talib (AS), kuwa walii na kiongozi wa Waislamu baada yake.

Siku hiyo Mtume (SAW) alitoa hotuba mbele ya hadhara kubwa ya Waislamu kisha akashika mkono wa Ali bin Abi Twalib na kusema: "Kila mtu ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali pia ni kiongozi wake.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran Hujjatul-Islam Kazem Seddiqi amesema katika hotuba za swala hiyo kwamba: "Ghadir ni ishara ya ukamilifu wa dini ya Uislamu na ramani ya njia ya jamii ya Kiislamu; na iliweka ajenda kuhusu mustakbali wa jamii ya Kiislamu."

Katika sehemu nyingine ya hotuba zake za Sala ya Ijumaa, Hujjatul Islam Seddiqi amesema kuwa: Uchamungu ni nguzo muhimu ya mwanadamu duniani na huko Akhera, na imeelezwa ndani ya Qur'an Tukufu kwamba yeyote anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu pia atamuondolewa mashaka na matatizo yake.

Vilevile amezungumzia umuhimu wa vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu na kusema vazi hilo humpa mwanamke heshima, sharafu na thamani.

4070968

captcha