IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi yamalizika Uganda

17:31 - May 08, 2022
Habari ID: 3475223
TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi wa shule na vyuo vikuu vya Uganda yamemalizika kwa kuzawadiwa washindi.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Tawi la Uganda la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uganda.

Mashindano hayo ya ambayo yamefanyika katika miezi ya Rajab na Ramadhani yalijumuisha shule na vyuo 40 kutoka maeneo yote ya Uganda.

Washiriki walishindana katika qiraa aina ya Tahqiq, Tarteel na kuhifadhi juzuu 10,20, na 30 za Qur'ani Tukufu na halikadhalika kuifashiri Sura al Hujurat kwa mujibu wa Tafsir al Mizan.

Sherehe za kufunga mashindano hayo zimehudhuriwa na maafsia wa ngazi za juu katika vyuo vikuu na halikadhalika balozi wa Iran nchini Uganda.

Akihutubu katika kikao hicho, Balozi wa Iran nchini Uganda Mehdi Salehi amepongeza jitihada za waandalizi wa mashindano na pia ameishukuru serikali ya Uganda kwa kulinda uhuru wa kuabudu nchini humo.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa ni chuo cha Kiislamu ambacho kilianzishw akwa lengo la kueneza mafundisho ya Kiislamu duniani kupitia mbinu na teknolojia za kisasa.

5484455

captcha