IQNA

Timu ya ‘fencing’ ya Libya yajiondoa mashindano ya dunia isichuane na Israel

12:20 - April 12, 2022
Habari ID: 3475116
TEHRAN (IQNA)- Timu ya kitaifa ya Libya ya mchezo wa kushindana kwa vitara au fencing imejiondoa katika ‘Mashindano ya Dunia ya Fencing’ ili kujizuia kukutana na timu ya utawala haramu wa Israel.

Mashindano hayo yanafanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu na tayari timu hiyo ya Libya ilikuwa imefika katika semi fainali.

Uamuzi huo umechukuliwa ili Libya isikutane na timu ya utawala haramu wa Israel katika fainali za mashindano hayo. Serikali ya Libya inapinga vikali uanzishwaji uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Libya ni ya pili barani Afrika katika mchezo wa kushindana kwa vitara au fencing na ni ya 19 duniani.

Katika miaka ya hivi karibuni wanariadha wa nchi za Kiislamu na Kiarabu wamekuwa wakikataa kushindana na wanariadha wa utawala haramu wa Israel kama njia ya kufungamana na Wapalestina ambao wanapigana kukomboa ardhi zao zinazokoloniwa na utawala wa Israel.

Hata baadhi ya wanariadha wa nchi za Kiarabu ambazo zimeanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel nao pia wamekataa kushindanoa na wanariadha wa utawala huo dhalimu.

4048689

captcha