IQNA

Katika safari ya rais wa Israel nchini UAE

Muungano wa UAE na utawala haramu wa Israel dhidi ya Yemen

10:54 - January 31, 2022
Habari ID: 3474872
TEHRAN (IQNA)- Rais Isaac Herzog wa utawala haramu wa Israel jana alifika Abu Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo alifanya mazungumzo mtawala wa Abu Dhabi Mohammad bin Zayed.

Katika kikao hicho Herzog alitangaza kufungamana na UAE katika vita dhidi ya Yemen huku akisema Israel itaipatia UAE misaada ya kijeshi kukabiliana na watu wa Yemen. 

Wakati huo huo, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, safari ya rais wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel nchini UAE ni chachu ya kuuhamasisha utawala huo utende jinai zaidi dhidi ya wananchi wa Palestina.

Rais wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Isaac Herzog leo amewasili Imarati kwa ziara rasmi, ambapo katika uwanja wa ndege alilakiwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Abdullah bin Zayed al Nahyan.

Harakati ya Hamas imeeleza katika taarifa kwamba, kuwakaribisha viongozi wa adui wa Kizayuni katika miji mikuu ya Kiarabu na Kiislamu ni zawadi kwa utawala huo ghasibu na ni kuushajiisha uendeleze jinai zake.

Taarifa hiyo ya Hamas imeongeza kuwa, inasikitisha kuona kwamba safari ya Herzog huko Abu Dhabi inafanyika sambamba na kushtadi mashambulio ya utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina kwa mauaji na kuwaweka kizuizini wananchi hao.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina imesisitiza katika taarifa yake kwamba, safari hizo za kimapatano na utawala wa Kizayuni zinaweza kuutia raghaba utawala huo ya kuzidisha hujuma na uchokozi wake dhidi ya watu wa Palestina.

Umoja wa Falme za Kiarabu ulisaini rasmi mkataba wa mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel tarehe 15 Septemba 2020 katika hafla iliyofanyika mjini Washington na kuhudhuriwa na rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump na hivyo kuutangaza rasmi na kuuweka hadharani uhusiano wake usio rasmi na wa miaka kadhaa na utawala huo haramu.

/4032552

captcha