IQNA

Kufa shahidi Balozi wa Iran nchini Yemen wakati wa mzingiro wa Saudia

21:23 - December 22, 2021
Habari ID: 3474709
TEHRAN (IQNA)- Kufa shahidi Hasan Irlu, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Sana'a kumedhihirisha ukubwa wa jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saud nchini humo.

Kufa shahidi Balozi wa Iran nchini Yemen wakati wa mzingiro wa Saudia

 

Takriban miaka saba imepita tangu muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulipoanzisha vita dhidi ya Yemen; na zaidi ya miaka mitano tangu Saudia ilipoiwekea mzingiro Yemen na kusitisha shughuli za uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sana'a. Ijapokuwa hadi sasa wananchi wa Yemen wameshaandamana mara kadhaa kulaani hatua ya Saudia ya kuiwekea mzingiro nchi yao na kutaka mzingiro huo uondolewe na shughuli za uwanja wa ndege wa Sana'a zianze tena, jambo ambalo limepigiwa kelele pia na baadhi ya asasi za kimataifa, lakini utawala wa Aal Saud umekataa kutekeleza takwa hilo. Siku ya Jumapili, kiongozi wa Ansarullah ya Yemen Abdulmalik al Houthi, alikosoa mwenendo huo wa Riyadh na akasema, Aal Saud umeifunga anga ya Sana'a lakini umezifungulia anga ya Saudi Arabia ndege za utawala  haramu wa Israel.

Tukio la kufa shahidi Hasan Irlu, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa mjini Sana'a, kwa mara nyingine tena limedhihirisha ukubwa wa jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Aal Saud. Siku mbili nyuma, Irlu, na baada ya kuwa mahututi, alisafirishwa kurejeshwa Iran kwa ndege iliyotumwa na serikali ya Iraq huko uwanja wa ndege wa Sana'a. Lakini hatua hiyo ilichukuliwa kwa kuchelewa; kwa sababu ni baada ya kuona balozi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yuko mahututi, ndipo Saudia ilitoa kibali cha kusafirishwa ili arejeshwe Iran. Saeed Khatibzadeh, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, shahidi Irlu, ambaye alikuwa majeruhi wa silaha za kemikali za wakati wa vita vya miaka minane viliavyoanzishwa na utawala wa Baath wa Iraq, alipatwa na ugonjwa wa corona Yemen alikopelekwa kikazi, lakini kwa masikitiko alirejea nchini akiwa katika hali mbaya kutokana na baadhi ya nchi kuchelewa kutoa ushirikiano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, naye pia amesema, baadhi ya nchi (Saudi Arabia) zilikwamisha mpango wa kumrejesha nchini Hassan Irlu ambaye alikuwa amepatwa na ugonjwa wa corona. Kwa hivyo moja ya vielelezo vya ukubwa wa jinai za utawala wa Aal Saud katika tukio hilo ni kuzuia kuruka ndege ya kumsafirisha Irlu, ambaye alikuwa afisa wa kidiplomasia mwenye kinga maalumu ya kisheria na ambaye ilipasa asafiri kuelekea nje ya Yemen kwa sababu alikuwa mgonjwa.

Nukta nyingine kuhusu ukubwa wa jinai hiyo ni kwamba, mzingiro wa pande zote iliowekewa Yemen na Saudia katika miaka hii ya karibuni, umeangamiza na kulemaza miundomsingi ya kiafya na kitiba ya nchi hiyo, kiasi kwamba wagonjwa wanashindwa kupatiwa matibabu; na hata uwezekano wa mtu kupata dawa ndani ya nchi hiyo pia hakuna. Kutokana na kukosekana suhula za matibabu, ilipasa Hasan Irlu, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Yemen, asafirishwe kuletwa Tehran; na hiyo ndiyo hali wanayokabiliana nayo pia raia wa kawadia wa Yemen. Hii ni pamoja na kwamba, mbali na maradhi angamizi ya Covid-19, watu wa Yemen wanasibiwa pia na aina zingine kadhaa za maradhi huku huduma za dawa na matibabu zikishindwa kupatikana nchini humo.

Kusambaa kwa maradhi, uhaba wa dawa na suhula za tiba na kuzuia wagonjwa wasisafarishwe kupelekwa nje ya Yemen kwa matibabu, ni sehemu ndogo tu ya athari hasi za sera ya mzingiro inayotokelezwa na utawala wa Aal Saud dhidi ya nchi hiyo. Lakini sera hiyo inasababisha maafa mengine pia, ambayo ni kujitokeza baa la njaa. Hadi sasa, asasi mbalimbali za kimataifa zimeshatoa indhari kuhusu baa la njaa linalowataabisha wananchi madhulumu wa Yemen; na hata Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hali mbaya ya kibinadamu iliyoko nchini humo ndio maafa makubwa zaidi ya kibinadamu katika karne hii ya 21.

Likini pamoja na yote hayo, Saudia haiko tayari kuchukua hatua yoyote ya kuifungua anga ya Sana'a; huku taasisi za kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa, nazo pia zikishindwa kuchukua hatua yoyote kivitendo ya kusitisha jinai hizo za Aal Saud. La kustaajabisha zaidi ni kuwa, Umoja wa Mataifa mpaka sasa umeshindwa hata kutoa kauli kuhusiana na kufa shahidi balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambaye alikuwa na kinga ya kisheria, kulingana na mikataba ya kisheria ya kidiplomasia..

3477044

 

Kishikizo: yemen irlu saudia
captcha