IQNA

Mpalestina apigwa risasi na askari dhalimu wa Israel

19:09 - September 01, 2021
Habari ID: 3474246
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala dhalimu wa Israel wamemuua shahidi kijana wa Palestina kwa kumpiga risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Kwa mujibu wa duru za habari Palestina, wanajeshi wa utawala haramu wa Israel walimpiga risasi barobaro huyo wa Kipalestina kwa jina la Raed Yousef Jadallah katika kijiji cha Beit Ur al-Tahta, magharibi mwa mji wa Ramallah.

Mashuhuda wanasema, baada ya kummiminia risasi kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 39, askari wa Israel walimuacha akavuja damu hadi akakata roho.

Wizara ya Afya ya Palestina imethibitisha kutoa mauaji hayo alfajiri ya leo Jumatano na kueleza kuwa, ni ya tatu ndani ya wiki moja huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Jumamosi iliyopita, kijana aliyekuwa na umri wa miaka 12 wa Kipalestina aliyefahamika kama Omar Hasan Abu an-Neel aliaga dunia kutokana na majeraha ya risasi za Wazayuni, katika mji wa Malka, mashariki mwa jiji la Gaza.

Haya yanajiri wiki mbili baada ya wanajeshi hao makatili wa utawala haramu wa Israel kuwaua shahidi vijana wanne Wapalestina kwa kuwapiga risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

3475599

Kishikizo: palestina israel mabavu
captcha