IQNA

Meli ya utawala wa Israel yahujumiwa Bahari ya Hindi

15:54 - July 04, 2021
Habari ID: 3474068
TEHRAN (IQNA)- Moto umezuka katika meli ya mizogo ya Israel baada ya kushambuliwa kwa 'silaha isiyojulikana' ikiwa katika maji ya Bahari ya Hindi.

Televisheni ya Al Mayadeen imesema meli hiyo ilikuwa njiani kuelekea katika bandari ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) iliposhambuliwa. Licha ya meli hiyo kusemekana kuwa ni ya Israel lakini viongozi wa utawala huo haramu wamesema wafanyakazi waliokuwemo hawakuwa raia wa utawala huo.

Televisheni ya N12 ya utawala wa Isreal imedai kuwa hakuna uharibifu mkubwa uliofanyika kwenye meli hiyo kufuatia shambulizi hilo na kwamba hakuna raia yeyote aliyejeruhiwa.

Mwezi Februari mwaka huu pia meli nyingine ya utawala wa Israel ilishambuliwa ikiwa katika maji ya Bahari ya Oman. Mwezi Aprili meli nyingine ya utawala huo ilishambuliwa katika pwani ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

3981768

Kishikizo: meli israel
captcha