Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kipindi hicho kilianza Jumamosi usiku kwa qiraa ya Qur’ani Tukufu ya Sura Nazi’at na Fajr ya Shahat Mohammad Anwar na leo usiku watazamaji wataweza kuona qiraa ya Sura al Muzzamil na Qiamah ya Mohammad Ahmad Shabeeb.
Aidha Januari 11 televisheni hiyo ya Qur’ani ya Iran itarusha hewani kwa mara ya kwanza qiraa ya Surah Naba, Tariq na Alaq ya Ustadh Ghalwash.
Televisheni ya Qur’ani ya Iran mara kwa mara hurusha hewani qiraa ya wasomi mashuhuri wa Misri.