Katika klipu ambayo imerushwa katika mitandao ya kijamii wawili hao wamesikika wakisema sehemu ya aya ya 29 ya Surah Al Fath katika Qur'ani Tukufu inayosema hivi: "Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao…"
Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kuwa Mtume Muhammad SAW alizaliwa 12 Rabiul Awwal nao Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kuwa ni 17 Rabiul Awwal.
Kwa msingi huo, Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya Umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa Waislamu kote duniani.