Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika sherehe iliyofanyika Jumamosi, mkurugenzi wa kituo hicho Dr Muhammad Babangida amesema waliohitimu, mbali na mafunzo ya Qur’ani, pia wamepata mafunzo ya sayansi ya kompyuta, hisabati na lugha ya Kiingereza.
Amesema wanafunzo hao wamepata ya kiwango cha juu na kwa vyeti walivyonavyo wanaweza kufunza Qur’ani katika nchi zote za Kiislamu duniani.
Aidha ametoa wito kwa wanachuo waliohitimu, ambao ni maarufu kama Alarammomi nchini Nigeria’ kutumia ujuzi waliopata kuimarisha maisha yao kijamii na kiuchumi.
Naibu mkuu wa chuo hicho Profesa Muhammad Bello naye ametoa wito kwa serkali za majimbo ya nchi hiyo kuwaajiri waliohitimu katika shule za umma ili kuongeza idadi ya waliohifadhi Qur’ani nchini humo.