Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo umefanyika katika
ukumbi mkubwa wa mikutano katika mji mkuu wa Guinea Conakry kwa kushiriki
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na himaya Ubalozi wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
Katika mkutano huo, zaidi wa maulamaa, wahubiri, maimamu na
mashekhe 1500 wa Ahul Sunna wal Jamaa, Mashia, na viongozi wa Tariqa ya
Tijaniyya kutoka kote Guinea Conakry walishiriki katika mkutano huo.
Kongamano hilo lilidhuhduriwa na Abdulkarim Chubati ambaye
ameitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa nchi yenye kueneza Umoja wa Kiislamu.
Aidha kikao hicho kilihutubiwa na Hujjatul Islam wal Muslimin
Dkt. Sayyid Mahmoud Waziri, mwakilishi
wa Ayatullah Makarim Shirazi na
Ayatullah Safi Golpaygani, marajii wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Dkt. Waziri ameashiria aya za Qur'ani Tukufu kuhusu umoja na
kusema moja ya nukta muhimu hivi leo ni umoja baina ya Waislamu.
Aidha mkutano huo ulihutubiwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Wasti, mwakilishi
wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu yenye makao yake
mjini Tehran.
3550314/