IQNA

Kifo cha Mustafa Ghalwash ni pigo kwa jamii ya Qur’ani

9:02 - February 09, 2016
Habari ID: 3470125
Qarii mtajika wa Misri amesema kifo cha hivi karibuni cha Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash, ni pigo kwa jamii ya wasomaji Qur’ani nchini humo.

Akizungumza na mwandishi wa IQNA, Ustadh Abdul Fattah Tarouti, ambaye binafsi ni qarii mashuhuri duniani, na amewahi kuwa jaji katika mashindano ya Qur’ani Iran, Saudia, Malaysia na Indonesia, ametuma salamu zake za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Sheikh Ghalwash na kusema kifo chake ni msiba mkubwa.

Sheikh Mustafa Ghalwash aliyekuwa qarii katika Radio ya Qur'ani ya Misri na mwanachama wa Jumuiya ya Wasomaji (quraa) na Waliohifadhi (huffadh) Qur'ani Misri aliaa dunia na kurejea kwa Mola wake mapema Alhamisi alfajiri akiwa na umri wa miaka 77 katika moja ya hospitali za Misri.

Ustadh Tarouti amesema Sheikh Ghalwash alikuwa miongoni mwa watangulizi wa mbinu mpya za qiraa ya Qur’ani Tukufu na kwamba kizazi cha sasa za quraa Misri walifaidika sana kutokana na ujuzi aliokuwa nao. Amesema Sheikh Ghalwash alikuwa kiunganishi baina ya kizazi cha zamani na cha sasa cha wasomaji Qur’ani. Amesema Sheikh Ghalwash alijifunza Qur’ani kutoka kwa Sheikh Mustafa Ismail.


3473569
captcha