IQNA

Ali Larijani

Madola ya magharibi yameunda Israel ili kuangamiza Uislamu

2:03 - July 11, 2015
Habari ID: 3326323
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, Ali Larijani amesema lengo kuu la nchi za Magharibi ni kuangamiza Uislamu na njama hiyo ilianzishwa Palestina.

Akihutubia halaiki kubwa ya waumini katika Swala ya Ijumaa mjini Tehran baada ya maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, Larijani amesema nchi za Magharibi ziliunda utawala bandia wa Israel katika ardhi za Palestina kwa lengo la kuvunja na kupora ardhi za Kiislamu. Spika wa Bunge la Iran ameongeza kuwa hitilafu baina ya baadhi ya nchi za Kiarabu ndio sababu ya kuendelea kubakia Israel. Larijani amesema ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979 ni jambo ambalo lilibadilisha startijia ya Waislamu katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Ijumaa ya leo ya tarehe 10 Julai, ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Waislamu na wapenda haki kote duniani wanaendelea na maandamano yao katika kona mbalimbali za dunia kuadhimisha siku hiyo muhimu ya kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina na Quds Tukufu.
Nchini Iran mamilioni ya wananchi wameshiriki katika maandamano hayo katika miji zaidi 770. Rais Hassan Rouhani wa Iran pia ameshiriki katika maandamano hayo mjini Tehran na kusema leo kunashuhudiwa hitilafu na magaidi katika nchi nyingi na hakuna shaka maovu hayo yanaungwa mkono na utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na madola ya kibeberu. Hata hivyo amesema Waislamu na Wapalestina wanaweza kufikia malengo yao wakiwa na umoja, mshikamano na mapambano .
Waandamanaji katika Siku ya Kimataifa ya Quds pia wametoa taarifa maalumu wakilaani kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu jinai za utawala haramu wa Israel. Aidha wamelaani vikali njama za Israel za Kuyahudisha ardhi za Palestina. Halikadhalika wamelaani jinai za kundi la Kitakfiri la ISIS huko Iraq, Syria na Libya na pia hujuma ya hivi sasa ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen. Wamesema hayo yote yanachochewa na utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na vibaraka wao kwa lengo la kuibua mifarakano baina ya Waislamu...mh

3326108

captcha