IQNA

Wazayuni wauhujumu tena Msikiti wa Al Aqsa, Wapalestina waitisha msaada

17:12 - February 24, 2015
Habari ID: 2891642
Walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Baitul Maqdis.

Duru zinaarifu kuwa leo Jumanne asubuhi, kwa mara nyingine walowezi hao wa Kizayuni wakiwa chini ya himaya ya askari wa utawala haramu wa Israel waliingia katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa wakipitia lango kuu la Babul Maghribiya. Wazayuni hao walivunjia heshima eneo hilo takatifu la Waislamu. Utawala wa Kizayuni unatekeleza njama za kuuyahidisha Mji wa Quds ikiwa ni pamoja na kuchimbua na kuharibu maeneo ya Msikiti wa Al Aqsa. Kufuatia hujuma hizo za mara kwa mara za Wazayuni, Wapalestina wametoa mwito kwa  Waislamu na wapenda haki kote duniani kuwasaidia kukabiliana na uchokozi huo wa Wazayuni.
Aidha Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuwazuia Wapalestina kuswali ndani ya Msikiti wa Al Aqsa huku wanawake na mabarobaro Wapalestina wakipokonywa vitambulisho vyao kabla ya kuruhusiwa kuingia ndani ya Msikiti. Hii ni katika hali ambayo walowezi wote wa Kizayuni wanaruhusiwa kuingia katika uwanja wa msikiti huo bila ya kizuizi chochote. Utawala wa Kizayuni wa Israel unatekeleza njama hatari ya kuuyahudisha mji wa Quds kwa kuwajaza walowezi wa Kizayuni katika eneo hilo sambamba na kuharibu maeneo ya kihisotria na kuwafukuza Wapalestina wenyeji wa eneo hilo. Msikiti wa Al Aqsa ndio sehemu ya tatu kwa utakatifu katika Uislamu baada ya Masjid al-Haram mjini Makka na Masjid al-Nabawi mjini Madina.../mh

2885771

captcha