Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya wafanyakazi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wametunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika Novemba 8.
2010 Nov 09 , 10:28
Sherehe za kutoa zawadi za mashindano ya kwanza ya kimataifa ya kuchapisha Qur'ani Tukufu zimefanyika leo mjini Tehran zikihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran Sayyid Muhammad Husseini.
2010 Nov 08 , 17:18
Maulamaa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Bahrain wameamua kujibu vitendo vya maadui wa Uislamu vya kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kuutangaza mwaka ujao wa 1432 Hijria kuwa mwaka wa 'kuwa pamoja na Qur'ani'.
2010 Nov 07 , 16:20
Raia watatu wa Uswisi waliokuwa na nia ya kuchoma moto nakala za vitabu vya Qur'ani Tukufu na Injili wametiwa nguvuni na polisi ya nchi hiyo.
2010 Nov 07 , 13:42
Mashidano ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 3-4 Disemba katika Chuo Kikuu cha Heights katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.
2010 Nov 07 , 12:56
Idara ya Wakfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq imetangaza majina ya washindi wa mashindano ya tatu ya kitaifa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya watu wenye vipaji.
2010 Nov 06 , 14:47
Baraza la Jiji la Tehran limetangaza kuwa linakusudia kujenga vyuo 373 vya Qur'ani (Dar-ul-Qur'an) katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2010 Nov 06 , 14:12
Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Visiwa vya Comoro wamezawadiwa katika hafla iliyofanyika Jumanne.
2010 Nov 04 , 12:01
Mashindano ya Kitaifa ya wanawake ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu yanatazamiwa kuanza Novemba 17 sawia na 10 Dhul Hijja, katika sikukuu ya Idul Adha mjini Tehran.
2010 Nov 04 , 11:56
Ujumbe wa wasomaji Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umeondoka Tehran Jumatano hii ukielekea katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
2010 Nov 04 , 11:53
Vitabu kuhusu miujiza ya kisayansi katika Qur'ani Tukufu vinaonyeshwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Sharjah.
2010 Nov 04 , 11:49
Taasisi ya kheri ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya mji wa Riyadh Saudi Arabia imeafiki kuanzishwa jumuiya ya kwanza ya kutayarisha walimu wa kuhifadhi Qur'ani makhsusi kwa ajili ya wanawake nchini humo.
2010 Nov 04 , 06:00
Zaidi ya wafungwa elfu sita katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamehifadhi Qur'an nzima au baadhi ya juzuu kufuatia juhudi za Idara ya Magereza nchini.
2010 Nov 01 , 18:03