Zaidi ya wafungwa elfu sita katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamehifadhi Qur'an nzima au baadhi ya juzuu kufuatia juhudi za Idara ya Magereza nchini.
2010 Nov 01 , 18:03
Kongamano la kwanza la kimataifa la utafiti wa Qur’ani limepangwa kufanyika tarehe 11 na 12 Januai mwakani katika mji wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.
2010 Nov 01 , 18:00
Wanachama wa Baraza la Uhakiki la al Azhar waliokutana hivi karibuni chini ya uenyekiti wa Sheikh Mkuu wa al Azhar Ahmad al Tayyib wamechukuwa uamuzi wa kuanzisha kiwanda cha kuchapisha Qur'ani tukufu.
2010 Oct 31 , 16:31
Iran ya Kiislamu ni muhuishaji wa Qur'ani na sayansi ya kitabu hicho na hii ndiyo nduvu iliyotajwa na Mwenyezi Mungu katika aya ya 60 ya suratul Anfal ya Qur'ani Tukufu akisema: "Na waandalieni nguvu mziwezao".
2010 Oct 31 , 16:05
Masomo ya muda mfupi ya kujifunza tafsiri ya Qur'ani Tukufu yataanza kutolewa katika Chuo Kikuu cha Sanaa cha mjini London Uingereza Jumamosi ya Tarehe 20 Novemba.
2010 Oct 31 , 11:39
Mashidano ya 16 ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Mafuta la Iran yelimalizika Ijumaa ya jana katika mji Mtakatifu wa Mash'had Kaskazini Mashariki mwa Iran.
2010 Oct 30 , 17:14
Mhadhiri mstaafu wa lugha za Kisemiti na utafiti wa masuala ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Bonn nchini Ujerumani amesisitiza juu ya udharura wa kutarjumiwa Qur'ani kwa lugha mbalimbali licha ya kukiri kwamba ni muhali kuweza kutarjumu kitabu hicho kikamilifu.
2010 Oct 30 , 13:51
Taasisi ya mafunzo ya Qur'ani ya Hamad bin Khalid itazinduliwa huko Doha mji mkuu wa Qatar mara tu baada ya kumalizika hija ya mwaka huu.
2010 Oct 30 , 13:20
Duru ya pili ya masomo ya kuhifadhi Qur’ani makhsusi kwa ajili ya wanawake wa Qatar imeanza ikisimamiwa na kitengo cha Qur’ani cha taasisi ya masuala ya kheri ya Iddi bin Muhammad Al Thani.
2010 Oct 30 , 13:14
Khalid bin Said al-Mushrifi, Mkurugenzi wa Idara ya Uhubiri wa Kidini ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Oman ametangaza habari ya kuzinduliwa hivi karibuni Msahafu wa Kitaifa wa nchi hiyo.
2010 Oct 28 , 12:12
Kikao cha kuchunguza Qur'ani Tukufu kilifanyika jana Jumatano tarehe 27 Oktoba katika maktaba kuu ya Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani.
2010 Oct 28 , 12:11
Katika mkutano na Mohammad Husseini Ahmadi Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Afrika Kusini, Yusuf Dadu Mkuu wa Kitengo cha Masomo ya Dini na Kiarabu Katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini amekaribisha pendekezo la Iran la kuandaliwa Wiki ya Qur'ani Tukufu nchini humo.
2010 Oct 28 , 12:02
Warsha ya Fasihi ya Q'ani na Taahira Yake katika Lugha ya Kiarabu itafanyika kesho Alkhamisi katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku. Warsha hiyo itahudhuriwa na wataalamu wa lugha ya Kiarabu na wanazuoni mashuhuri.
2010 Oct 27 , 15:10