Masomo ya 'fikra za kiufumbuzi katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu' yalianza siku ya Alkhamisi huko Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania.
2010 Dec 04 , 13:46
Taasisi ya Qur'ani ya As-Shatibi ya Kuwait siku ya Alkhamisi ilifungua kituo chake cha kumi cha kuendeshea mafundisho ya Qur'ani ambacho ni maalumu kwa wanawake katika eneo la al-Jahra.
2010 Dec 04 , 13:36
Qari Mashuhuri wa Misri Ustadh Farajullah Shazli amesifu maafisa wa Iran kutokana na juhudi zao za kustawisha shughuli za Qurani na kusema uungaji mkono wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni nukta muhimu zaidi katika kuenea shughuli za Qurani nchini Iran.
2010 Dec 01 , 22:04
Mwakilishi wa Libya katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Mash'had:
Kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika kiwango cha wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu kunachangia mno katika kueneza na kuimarisha zaidi utamaduni na thamani za Kiislamu na kustawisha zaidi uhusiano kati ya nchi za Waislamu.
2010 Dec 01 , 12:47
Mkutano wa 'Uislamu kwa ajili ya Amani' mjini Doha Qatar umesisitiza kwamba Uislamu unapasa kutambuliwa na kufahamika kupitia Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume (saw) na kwamba haupaswi kupimwa kwa tabia na misimamo ya watu.
2010 Nov 30 , 17:04
Kikao cha kuchunguza njia bora za kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu, kanuni za lugha ya Kiarabu na sheria za Kiislamu kwa kizazi kipya cha Waislamu waliowachache nchini Uingereza kimepangwa kufanyika katika Kituo cha Kiislamu cha London.
2010 Nov 30 , 16:51
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema anaunga mkono hatua ya Bunge ya kuongeza kipengee kuhusu shughulu za Qur'ani katika kitengo cha utamaduni cha Mpango wa Tano wa Maendeleo.
2010 Nov 30 , 07:29
Maonyesho ya kwanza ya nuskha za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa mkono yalianza siku ya Jumamosi katika msikiti wa Amran bin Shaheen katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq.
2010 Nov 29 , 17:24
Fainali ya mashindano ya 24 ya Qur'ani ya wafanyakazi wa kitengo cha anga za juu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, inatazamiwa kufanyika Januari 3-5 mwaka 2010.
2010 Nov 29 , 16:39
Taasisi ya masuala ya kheri ya Darul Birr ya Dubai katika Umoja wa Falme wa Kiarabu imetoa zawadi ya nakala elfu ishirini za Qur’ani Tukufu kwa nchi kadhaa za Kiafrika.
2010 Nov 29 , 14:50
Duru ya Saba ya Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani yanaaza alasiri leo Novemba 28.
2010 Nov 28 , 14:22
Sambamba na Sikukuu ya Eid-ul-Ghadir, washiriki walioshinda katika Duru ya Pili ya Darsa ya Kiraa ya Qur'ani kwa vijana Zambia wametunukiwa zawadi.
2010 Nov 28 , 14:20
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW cha Qum nchini Iran kimeanzisha vituo 110 vya Qur'ani –Dar-ul-Quran- katika zaidi ya nchi 50 duniani.
2010 Nov 28 , 08:35