Makarii na mahafidh 30 wa Qur’ani Tukufu walichuana jana Jumanne katika siku ya pili ya Mashindano ya Kimataifa Qur’ani Tukufu yanayoendelea nchini Saudi Arabia.
2010 Dec 29 , 14:10
Kushiriki wanawake katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yaliyopangwa kufanyika nchini Iran na kuanzishwa vitengo vipya kama vile ufahamu wa Qur'ani, adhana na qaswida ni mambo yatakayoiunua kiwango cha mashindano.
2010 Dec 29 , 13:19
Mahafidh kadhaa wa Qur'ani Tukufu wameenziwa katika sherehe maalumu iliyofanyika katika mji wa Bensberg nchini Ujerumani kwa udhamini wa sekretarieti ya Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Sharja, moja ya Falme za Kiarabu zinazounda Imarati.
2010 Dec 29 , 13:07
Mfuko wa kuwahami walimu wa Qur'ani Tukufu wa Saudi Arabia umeanzishwa na Amir wa Makka Khalid Faisal.
2010 Dec 28 , 17:07
Mafunzo ya muda ya Qur'ani na maarifa ya kitabu hicho makhsusi kwa watoto wadogo yataanza kutolewa mwaka mpya wa 2011 katika Taasisi ya Utafiti wa Sheria za Kiislamu katika eneo la Heideveld katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini.
2010 Dec 28 , 16:53
Duru ya 13 ya mashindano ya kila mwaka ya hifdhi, tilawa na tafsiri ya Qur'ani Tukufu inaendelea nchini Lebanon.
2010 Dec 28 , 13:05
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu wa Macho Katika Ulimwengu wa Kiarabu Khalid Ali Al Naimy ametoa zawadi ya Qur'ani ya braili kwa Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Qatar Ghaith bin Mubarak bin Imran Al Kuwari.
2010 Dec 28 , 13:01
Sheikh Saleh Bin Abdulaziz Al Sheikh Waziri wa Masuala ya Kiislamu nchini Saudi Arabia ameshiriki katika sherehe za kufungua Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani mjini Makka na kusisitiza juu ya nafasi ya Qur'an katika Umoja wa Kiislamu.
2010 Dec 28 , 12:58
Kikao cha mafunzo cha kufasiri sura tukufu ya al Hadid kimepangwa kufanyika tarehe 15 Januari katika Chuo Kikuu cha London.
2010 Dec 27 , 17:36
Sherehe za kuwaenzi makarii na mahafidha wa Qur'ani Tukufu huko Palestina zimefanyika katika mji wa Ramallah.
2010 Dec 27 , 16:46
Mashindano ya Kimataifa ya 32 ya Qur’ani Tukufu ya Saudi Arabia yameanza leo Jumatatu katika nyanja za hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur’ani Tukufu. Mashindno hayo yanayofanyika katika mji mtakatifu wa Makka yanarushwa hewani moja kwa moja kupitia Redio Qur’ani ya Saudia.
2010 Dec 27 , 14:00
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri imepinga hatua ya mtafiti na mwandishi mmoja wa Kikristo ya kutaka kutarjumu Qur'ani Tukufu katika lugha ya Kiamazighi.
2010 Dec 27 , 10:48
Mashindano ya 32 ya kimataifa ya kusoma, hifdhi na kufasiri Qur'ani Tukufu yataanza kesho tarehe 26 Disemba katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia.
2010 Dec 25 , 16:41