Kitengo cha Kimataifa katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani Tehran kinafunguliwa Jumatano ya leo katika hafla itakayohudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran na vilevile mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu.
2011 Aug 10 , 13:21
Benki ya Maendeleo ya Kiislamu BID jana Jumatatu ilichukua uamuzi wa kutenga franka bilioni 9 kwa ajili ya kukarabati shule na madarsa za Qur'ani nchini Senegal.
2011 Aug 09 , 17:11
Mashindano ya 7 ya Hifdhi na Kiraa ya Qur’ani Tukufu yaliyopewa jina la “Mazamir Aal Daud” yalianza jana huko Sharja katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
2011 Aug 09 , 15:27
Vikao vya kufarijika na Qur'ani ambavyo tokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Ramadhani vimekuwa vikifanyika katika Haram mbili za Imam Hussein na Hadhrat Abbas (as) huko katika mji mtakatifu wa Karbala viliendelea hapo jana Jumapili ambapo Ahmad Nuina, msomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Misri alishiriki.
2011 Aug 08 , 19:48
Kufikia sasa zaidi ya tarjumi 1200 za Qur'ani zilizotarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi zimegunduliwa.
2011 Aug 08 , 19:45
Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya viziwi yameanza leo Jumatatu nchini Kuwait na yataendelea hadi Jumatano Agosti 10.
2011 Aug 08 , 19:42
Kikao cha ‘Mbinu ya Ahul Bayt AS katika kutafsiri Qur’ani’ kinafanyika Jumatatu hii katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tehran.
2011 Aug 08 , 14:21
Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Misri yanatazamiwa kuanza tarehe 19 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2011 Aug 08 , 14:17
Mashindano ya 15 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai yameanza katika Kituo cha Utamaduni na Sayansi katika eneo la Al Mamzar Dubai huko Umoja wa Falme za Kiarabu.
2011 Aug 08 , 14:14
Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu, imeyaarifisha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai kuwa mashindano bora zaidi ya Qur'ani katika mwaka huu wa 2011 unaosadifiana na mwaka 1432 Hijiria.
2011 Aug 07 , 17:13
Nakala ya kwanza ya maandishi ya mkono ya Qur'ani Tukufu ambayo iliandikwa miaka 70 baada ya kufariki dunia Mtume Muhammad SAW inahifadhiwa katika Msikiti wa Jamia wa Sanaa nchini Yemen.
2011 Aug 07 , 15:46
Chumba cha Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya Iran katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran kimearifisha tarjumi za Qur'ani kwa lugha mbalimbali ambazo zimechapishwa nchini Iran.
2011 Aug 07 , 14:49
Awamu ya pili ya mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi yamefanyika katika eneo la Ashanti nchini Ghana katika siku za awali za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2011 Aug 07 , 14:26