Kamusi kubwa zaidi ya Qur'ani Tukufu iliyopewa jina la "Kamusi ya Qur'ani" imetarjumiwa kwa lugha ya Kiingereza mjini London. Kamusi hiyo imetarjumiwa kwa ushirikiano wa Chuo cha Kiislamu cha London.
2009 Feb 18 , 11:36
Giniyev Ganev ambaye ni miongoni mwa mawakili wa Bulgaria amesema kuwa Qur'ani Tukufu ni miongoni mwa vitabu adhimu katika historia ya mwanadamu na kuongeza kuwa hajawahi kuona ishara yoyote ya wito wa vitendo vya kigaidi na utumiaji mabavu katika Qur'ani.
2009 Feb 17 , 17:13
Mahakama ya Rufaa ya Afghanistan imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela Waafghani wawili kwa kutarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiafghani bila ya matini yake ya Kiarabu ambayo wameiita "Qur'ani Safi."
2009 Feb 17 , 17:11
Mshindi wa sehemu ya tarjumi ya Qur'ani Tukufu ya duru ya 16 ya zawadi ya kimataifa ya kitabu cha mwaka amesema kuwa ametumia miaka 40 ya umri wake kwa ajili ya kutarjumi Qur'ani kwa lugha ya Kijerumani kwa shabaha ya kutoa tarjumi iliyojengeka juu ya uhakika na upendo wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu ili wasiokuwa Waislamu wakisome kama wakisamavyo Waislamu.
2009 Feb 16 , 18:53
Qur'ani Tukufu ndio ufumbuzi wa hitilafu za umma wa Kiislamu na ufunguo wa ufanisi wa mwanadamu. Vilevile Waislamu wote wanaweza kuungana kwa msaada wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
2009 Feb 16 , 16:05
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanjan:
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanjan nchini Iran Hujjatul Islam Ali Ridha Mehranfar amesema mghafala na kutomkumbuka mwenyezi Mungu kunamzuia mja kufikia maisha ya saada na ufanisi kwa mtazamo wa Qur'ani.
2009 Feb 15 , 14:11
Hatua ya mwisho ya mashindano ya pili ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu ya Zawadi ya Dubai yameanza leo mjini humo na yataendelea hadi tarehe 23 Februari.
2009 Feb 15 , 09:58
Muda wa kujiandikisha kushiriki katika Olimpiadi ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani na Hadithi iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha "Jamiatul Mustafa (SAW) al Alamiya" umeongezwa hadi tarehe 18 Februari.
2009 Feb 12 , 19:00
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanjan:
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanjan nchini Iran Hujjatul Islam Ali Ridha Mehranfar amesema mghafala na kutomkumbuka mwenyezi Mungu kunamzuia mja kufikia maisha ya saada na ufanisi kwa mtazamo wa Qur'ani.
2009 Feb 11 , 15:22
Tovuti mpya ya Jumuiya ya Qur'ani ya Mfalme Fahd imezinduliwa katika mji mtakatifu wa Madina kwa lengo la kuwasilisha Qur'ani Tukufu kwa miandiko mbalimbali ya Kompyuta.
2009 Feb 11 , 15:20
Mtalii mmoja wa Sweden katika eneo la Kashmir ambaye alibandika aya za Qur'ani Tukufu juu ya relitheluji zinzotumiwa katika mchezo wa ski, amewaomba radhi Waislamu.
2009 Feb 11 , 13:28
Wanasesera wa Kiislamu wataanza kuuzwa katika maduka makubwa ya Asda ya Uingereza mwezi ujao kwa ajili ya kuwafundisha watoto wa Kiislamu istilahi na maana ya sura za Qur'ani Tukufu.
2009 Feb 09 , 09:55
Nakala ya Qurani ya pili kwa kuwa na umbo dogo zaidi duniani ambayo ina umri wa miaka 117 inahifadhiwa katika mji wa San'aa huko Yemen.
2009 Feb 08 , 10:06