Mashindano ya kila mwaka ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu yanatazamiwa kufanyika katika wiki ya mwisho ya mwezi Julai mwaka huu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
2009 Apr 06 , 16:27
Mkutano wa Wakurugenzi wa jumuiya za Qur'ani Tukufu za eneo la Ulaya Mashariki na Uturuki wamekutana katika mji mkuu wa Uturuki Istanul. Mkutano huo unasimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
2009 Apr 06 , 15:35
Dini tukufu ya Kiislamu imesisitiza mno juu ya udharura wa kutafuta elimu na maarifa kwa Waislamu. Tiba ni moja kati ya mambo yaliyozungumziwa katika Qur'ani Tukufu na hadithi. Kutokana na umuhimu wa mitazamo ya Qur'ani kuhusu tiba na afya, hadi sasa kumefanyika vikao na mikutano mbalimbali katika medani ya elimu ya tiba katika mtazamo wa Qur'ani.
2009 Apr 06 , 12:18
Idara inayohusika na masuala ya utafiti katika Chuo Kikuu cha Imam Swadiq(as) imeanzisha mradi wa kuagiza, kupokea na kusambaza vitabu bora vinavyohusiana na Qur'ani Tukufu, ikiwa ni katika juhudi zake za kuimarisha na kueneza utafiti wa Qur'ani unaokwenda sambamba na jamii ya sasa.
2009 Apr 06 , 08:56
Toleo la 34 la jarida la masuala ya Qur'ani la Kashila kwa maana ya "Mawaidha" ambalo linajadili maisha ya Nabii Muhammad (saw) limechapishwa nchini Albania kwa lugha ya Shqip.
2009 Apr 05 , 11:24
Majmui ya nakala za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa hati za mkono za Kituo cha Uhakiki cha Chuo Kikuu cha Addis Ababa zimetayarishwa na kuhifadhiwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.
2009 Apr 05 , 11:22
Ubalozi wa Kuwait mjini Brussels Ubelgiji umepanga kuandaa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani nchini humo tarehe 18 Aprili, kwa jina la Swabah Ahmad al-Jabir as-Swabah.
2009 Apr 04 , 17:54
Filamu ya matukio ya kweli (Documentary) kuhusu misikiti ya Paris inatarajiwa kuonyeshwa mjini Marseille tarehe kumi Aprili.
2009 Apr 04 , 15:14
Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa serikali halali ya Palestina Twalib Abu Shir amesema kuwa kanali ya televisheni ya satalaiti ya Qur'ani Tukufu itafunguliwa katika eneo la Gaza.
2009 Apr 04 , 11:19
Sherehe za kuwatunuku zawadi washiriki katika mashindano ya taifa ya Qur'ani makhsusi kwa watoto wadogo, zimefanyika leo mjini Riyadh Saudi Arabia.
2009 Mar 30 , 15:06
Waziri wa Masuala ya Kidini wa Indonesia ameitaka mirengo mbalimbali ya kisiasa nchini humo kutotumia aya za Qur'ani kama wenzo wa kampeni za uchaguzi.
2009 Mar 28 , 13:37
Huku akiashiria umashuhuri wa Mustafa Ismail katika usomaji wa Qur'ani Tukufu, mmoja wa shakhsia muhimu katika uwanja huo amemsifu sana msomaji huyo muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu na kusisitiza kwamba, alianzisha mbinu mpya katika lahani za usomaji Qur'ani na hivyo kufuatwa na wasomaji wengi katika uwanja huo.
2009 Mar 26 , 20:41
Msomaji mmoja wa kimataifa wa Qur'ani Tukufua amesifu usomaji wa marehemu Mustafa Ismail na kusema kuwa lahani zake tofauti katika usomaji wa kitabu hicho kitakatifu zinaonyesha wazi umahiri na ustadi mkubwa aliokuwa nao katika usomaji wa Qur'ani.
2009 Mar 26 , 20:26