Awamu ya kwanza ya mashindano ya taifa ya kuhifadhi Qur'ani katika Umoja wa Falme wa Kiarabu ilimalizika jana.
2009 Apr 14 , 15:09
Suala la kuweka wazi vigezo vya marekebisho ya matumizi ya mwanadamu ni jambo la dharura ambalo limefafanuliwa kwa njia bora zaidi katika aya za Qur'ani Tukufu.
2009 Apr 14 , 14:49
Qur'ani Tukufu inayonasibishwa kwa Imam Mussa al Kadim (as) ambaye ni mmoja wa Maimamu Watukufu kutoka Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) ni nakala yenye thamani kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na dhihirisho la sanaa ya Kiislamu na Iran.
2009 Apr 14 , 13:55
Somo la Qur'ani, historia yake na sayansi ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu litaanza kufundishwa katika Chuo cha Teolojia cha Kanisa Katoliki nchini Zambia. Somo hilo litatolewa na Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Lusaka Asadi Muwahhid.
2009 Apr 13 , 14:42
Mashindano ya 11 ya taifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la Amir Sulaiman yamepangwa kufanyika baadaye mwezi huu nchini Saudi Arabia.
2009 Apr 12 , 11:55
Mashindano ya kumi ya taifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yameanza leo nchini Imarati yakisimamiwa na Idara ya Masuala ya Kiislamu ya Dubai.
2009 Apr 12 , 00:53
Washiriki katika kongamano la Wakurugenzi wa vituo vya Qur'ani katika nchi za Ulaya Mashariki wanaokutana mjini Istanbul Uturuki wametoa wito wa kuasisiwa jumuiya ya wasomaji Qur'ani katika eneo hilo.
2009 Apr 11 , 14:04
Mashirika ya uchapishaji ya Omega 2001 na One Press ya nchini Marekani yanayojulikana kwa jina bandia la Swafa na al-Mahdi yamechapisha Qur'ani bandia kwa jina la al-Furqan al-Haq na kuisambaza nchini Kuwait ikiwa ni njama nyingine za kupotosha kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
2009 Apr 09 , 11:59
Kiwango cha utafiti wa masuala ya Qur’ani ni cha chini sana ikilinganishwa na utafiti uliofanywa hadi sasa kuhusiana na vitabu vingine vya mbinguni hususan Taurati na Injili, na kwa msingi huo ulimwengu wa Kiislamu unapasa kufanya jitihada kubwa zaidi za kustawisha na kupanua utafiti wa Qur’ani.
2009 Apr 08 , 17:11
Mashindano ya taifa ya kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu yaliyopewa jina la “al Dhikrul Hakim” yanatarajiwa kuanza tarehe 17 Aprili nchini Bahrain.
2009 Apr 08 , 17:09
Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya kuchagua washiriki wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yanatazamiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu wa Aprili.
2009 Apr 07 , 17:02
Tarjumi kamili ya Qur'ani Tukufu imeanza kusambazwa na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania.
Tarjumi hiyo imeandikwa na Sheikh Ali Juma Mayunga na kuhaririwa na Taasisi ya Ansariyan mjini Qum nchini Iran.
2009 Apr 07 , 17:00
Mashindano ya kila mwaka ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu yanatazamiwa kufanyika katika wiki ya mwisho ya mwezi Julai mwaka huu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
2009 Apr 06 , 16:27