Mpango wa Kusoma Qur'ani Tukufu katika mtandao wa intaneti wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu mjini Washington Marekani umewavutia wengi.
2009 May 04 , 08:49
Maonyesho ya nakala za kale na za kihistoria za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za waandishi na wanafikra wakubwa wa Kiislamu ikiwemo nakala iliyoandikwa kwa hati za Imam Sajjad, mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), yameanza katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq.
2009 May 04 , 07:57
Mashindano ya sauti nzuri zaidi ya kisomo cha Qur'ani Tukufu yanaanza leo katika mji wa Dubai kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu. Mashindano hayo yanasimiwa na kamati inayosimamia mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Zawadi ya Dubai.
2009 May 03 , 09:49
Mpango wa kuhifadhi Qur'ani wa al Shafii' umetekelezwa katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu katika kituo cha Darul Qur'ani.
2009 May 03 , 09:47
Watoto wadogo wanapaswa kufunzwa Qur'ani Tukufu kwa kutilia maanani mambo yanayowavutia kama michoro, visa na kadhalika.
2009 May 01 , 00:39
Wadau nchini Iran wameazimia kuinua kiwango cha vipindi vya redio na kanali ya televisheni ya Qur'ani kwa kutumia Maqari mahiri na wenye vipawa.
2009 Apr 30 , 15:43
Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Thailand, Jalal Tamleh ametembelea Kituo cha Qur'ani cha Rasul A’adham (SAW) kinachofungama na Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa (SAW) al Alamiya.
2009 Apr 30 , 15:39
Wasomi, watafiti na wanachuo wanaokusudia kutuma makala katika mashindano ya 26 ya kimataifa ya Quran Tukufu ya Iran wanaweza kutuma makala zao kupitia njia ya intaneti.
2009 Apr 29 , 13:21
Qur'ani Tukufu na mafundisho yake imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali za wapinzani wa Uislamu na changamoto hizo zimeongezeka zaidi katika zama za sasa zinazotambuliwa kuwa ni zama za mapinduzi ya mawasiliano.
2009 Apr 29 , 13:01
Sekretarieti ya Wizara ya Waqfu ya Kuwait imengaza kuwa muhula wa kujiandikisha kwa ajili ya mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani yatakayofanyika chini ya anwani ya "Hii Ndiyo Nguzo Yangu", unakaribia kumalizika.
2009 Apr 29 , 12:33
Mashindano wa 22 ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu chini ya anuani ya "Abdulazizi bin Muhammad Al Khalifa" yameanza nchini Bahrain.
2009 Apr 28 , 13:26
Tovuti ya masuala ya kiitikadi, kisiasa na kiutamaduni ambayo huakisi shughuli za Idara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran inayoshughulikia masuala ya vyuo vikuu nchini imetunga leksikografia (usanidi kamusi au mu'jam) ya Qur'ani kupitia mtandao.
2009 Apr 28 , 13:22
Mjumuiko wa CD za visomo vya maqari mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu umekusanywa katika benki ya sauti na taswira katika Haram Takatifu la Abdul Adhim al Hassani (as) kusini mwa jiji la Tehran.
2009 Apr 26 , 09:43