Wiki ya kuadhimisha Qur'ani Tukufu ilianza kutekelezwa siku ya Jumapili katika miji tofauti ya Palestina. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Taasisi ya al-Furqan ya nchi hiyo.
2009 May 19 , 11:01
Idara ya Waqfu ya mkoa wa Rasifat nchini Jordan imetangaza kuwa itaandaa vikao vya mafundisho ya kuhifadhi na kusoma Quran Tukufu wakati wa mapumziko katika msimu ujao wa joto.
2009 May 18 , 14:09
Kambi ya wanafunzi 2000 waliotia fora katika mashindano ya Quran na Sala mwaka huu watashiriki katika kambi maalumu masomo ya Quran katika mji mkuu wa Iran, Tehran mwezi Julai.
2009 May 18 , 14:08
Kumetangazwa mashindano ya uandishi makala kuhusu Quran kama mojawapo wa shughuli za pembizoni mwa mashindano ya kimataifa ya Quran Tukufu nchini Ghana.
2009 May 18 , 14:08
Duru za masomo ya Qur'ani maalumu kwa vijana wa kike na kiume wa Pakistan zitaanza hivi karibuni katika eneo la milimani la Gilgit lililoko kaskazini mwa nchi hiyo.
2009 May 16 , 17:02
Mashindano ya Kaligrafia ya Aya za Quran Tukufu yamefanyika katika mji mkuu wa Bahrain Manama na kuwashirikisha wasanii 20.
2009 May 16 , 14:18
Vituo viwili vipya vya mafunzo ya Quran Tukufu vijulikanavyo kama 'Sayyeda Ruqaiya (SA) ' na 'Abdulla bin al Hussein (AS) vimefunguliwa na Taasisi ya Misaada ya Imam Ali (AS) chini ya usimamizi wa Ayatollah Mohammad Taqi Modarresi, mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kishia katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq.
2009 May 16 , 14:17
Kitabu cha ad-Dilalatul Qur'aniyatu fi Fikri Muhammad Hussein Tabatabai ambacho kina kurasa 346 na kilichoandikwa na mwandishi wa Lebanon kimeonyeshwa katika kibanda cha Darul Huda Litabaa' wa Nashril wa Tauzi' ya Lebanon katika maonyesho ya kimataifa yanayooendelea mjini Tehran.
2009 May 14 , 14:14
Duru maalumu za mafunzo ya usomaji Qur'ani na tajweed maalumu kwa walifu wa Qur'ani zilianza kutekelezwa jana Jumanne huko Islamabad mji mkuu wa Pakistan.
2009 May 13 , 11:20
Ayatollah Mohammad Taqi Modaressi, mwanazuoni mwandamizi wa Kishia amesema kuheshimu haki na rai za watu katika jamii ni kati ya sifa za muhimu za jamii ya Kiislamu ambazo huipa itibari jamii inayofuata mafundisho ya Quran.
2009 May 12 , 13:58
Kundi la kwanza la Mahafidh wa Qur'an Tukufu limekamilisha masomo na kufuzu katika Msikiti wa Hafidh Ali huko Istanbul Uturuki.
2009 May 12 , 12:31
Duru ya 75 ya mashindano ya kitaifa ya masomo ya Qur'ani Takatifu, imeanza siku ya Jumamosi nchini Saudi Arabia. Duru hiyo ya masomo inadhaminiwa na Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya na Kuhifadhi Qur'ani katika mkoa wa Taif.
2009 May 10 , 09:42
Msomaji mmoja mashuhuri wa Qur'ani nchini Iran anaamini kwamba mazoezi ya kudumu ya usomaji wa kitabu hicho humfanya msomaji kuwa na kipawa cha na uwezo wa kudhibiti usomaji wa kitabu hicho kitakatifu.
2009 May 10 , 09:39