Tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha 13 pamoja na tarjumi 6 mbalimbali kwa lugha ya Kiingereza na tarjumi 9 mbalimbali kwa lugha ya Kifarsi zimewasilishwa katika programu ya kompyuta ijulikanayo kama "Nasim Ridhwan" katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran.
2010 Aug 24 , 12:54
Kitengo cha tarjumi ya Qur'ani Tukufu katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kimefanikiwa kuarifisha tarjumi za Qur'ani Tukufu kwa lugha 112 za dunia.
2010 Aug 24 , 12:48
Nafasi muhimu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Wairani katika kueneza tafsiri na mafundisho ya Qur'ani Tukufu imebainishiwa wageni wanaoyatembelea Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran.
2010 Aug 24 , 12:36
Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu ya 'Zawadi ya Dubai' yanaendelea leo Jumatatu ambapo washiriki 7 kutoka Uingereza, Tunisia, Oman, Uzbekistan, Visiwa vya Comoro na Gambia watashindana.
2010 Aug 23 , 15:42
Maonyesho ya Qur’ani Tukufu katika Kioo cha Sanaa yamepangwa kufanyika Alkhamisi ya wiki hii katika makao ya Jumuiya ya Wapiga Picha wa Qatar katika eneo la al Hilal mjini Doha.
2010 Aug 23 , 15:32
Awamu ya tatu ya mashindano ya kusoma Qur’ani makhsusi kwa wanaume imeanza Jumatatu ya leo katika mji mkuu wa Imarati Abu Dhabi.
2010 Aug 23 , 15:13
Jumuiya ya masuala ya kheri ya Wa'tasamu ya Libya imetangaza maudhui za mijadala ya vikao vya taaluma ya Qur'ani vitakavyofanyika pambizoni mwa Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu makhsusi kwa wanawake ya jumuiya hiyo.
2010 Aug 22 , 16:00
Viongozi wa dini mbalimbali katika jimbo la Florida huko Marekani wanakusudia kujibu uamuzi uliochukuliwa na kanisa la The Dove World Outreach Center la mji huo wa kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kuitisha kongamanao la "Amani na Matumaini".
2010 Aug 22 , 15:59
Mashindano ya kwanza ya kila mwaka ya utafiti katika Qur'ani Tukufu, maalumu kwa familia za Kiislamu zinazoishi nchini Marekani yatafanyika hivi karibuni mjini New York.
2010 Aug 22 , 11:41
Duru ya 15 ya mashindano ya kusoma na kufasiri Qur'ani Tukufu ambayo yamekuwa yakiendelea huko Manama mji mkuu wa Bahrain yamepangwa kumalizika tarehe 27 ya mwezi huu wa Agosti.
2010 Aug 22 , 11:33
Vipindi vya 'Fikra za Qur'ani' vimekuwa vikitangazwa katika televisheni ya satalaiti ya Fourteen ya nchini Bahrain kwa ajili ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
2010 Aug 21 , 15:24
Viongozi wa serikali katika jimbo la Florida nchini Marekani wamekataa ombi la makasisi wa Kikristo wanaopiga vita Uislamu la kutoa kibali cha kuchomwa moto Qur'ani kadamnasi na mbele ya halaiki ya watu.
2010 Aug 21 , 15:17
Mashindano ya kila mwaka ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa mbinu ya tajweed yanayojulikana kwa jila la Hilal yameanza leo Jumamosi mjini Riadh Saudi Arabia.
2010 Aug 21 , 15:14